in

Facebook Yaunganisha Instagram DM na Messenger

kwa sasa bado iko kwenye majaribio na itakuja kwa watumiaji wote hivi karibuni

Facebook Yaunganisha Instagram DM na Messenger

Kampuni ya Facebook imetangaza kuwa hivi karibuni itazindua sehemu mpya ya kuchat kupita Instagram, sehemu ambayo itakuwa na sehemu nyingi zaidi kuliko sehemu ya sasa na itakuwa na muungano wa Facebook Messenger pamoja na Instagram DM au Direct Messages.

Sehemu hiyo mpya ya Instagram DM inakuja na sehemu mpya kama vile Stickers, meseji zinazo jifuta zenyewe (Vanishing messages), selfie stickers, custom emoji, chat colors, njia mpya ya kuzuia meseji kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na njia mpya ya kuangalia video kwa pamoja ukiwa unawasiliana na mtu kwa njia ya video, (watch together) iliyo zinduliwa hivi karibuni.

Mbali na hayo, muunganiko huo pia utaruhusu watumiaji wa instagram kuweza kufafuta akaunti mbalimbali kutoka kwenye mitandao yote miwili kwa wakati mmoja, yaani mtumiaji ataweza kutafuta majina kupitia Messenger na pia kupitia Direct Message kwa pamoja.

Hata hivyo inasemekana kuwa, sehemu hiyo na nyingine zitakuwa ni chaguo la mtu, kama mtu haitaji kuunganisha app hizo mbili basi anaweza kusitisha kwa kukataa kuunganisha sehemu hizo mbili za DM na FB Messenger.

Jinsi ya Kusajili Biashara Kupitia Google My Business (2023)

Kwa sasa sehemu hiyo bado ipo kwenye hatua za majaribio na inategemea kuja kwa watumiaji wote siku za karibuni. Kama unataka kuwa wa kwanza kujaribu sehemu hii, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.