in

Fungua Application Yoyote ya Android kwa Kutumia SMS

Utaweza pia kufanya mambo mengine kama kuzima simu kwa kutumia SMS

Fungua Application Yoyote ya Android kwa Kutumia SMS4:53

Ukweli ni kwamba simu nyingi ni “Smartphone” lakini simu zenyewe bila kuwepo kwa application sidhani kama simu zingekuwa Smart.

Moja kati ya app ambayo inafanya simu kuwa Smart ni App hii ya Automateit, App hii ina uwezo wa kufanya mambo mengi sana ambayo mengine ulikua hujui kama yanawezekana kwenye simu yako ya Android.

Kwa kuanza leo nimekuletea njia hii fupi ambayo unaweza kutumia App ya Automateit kuweza kufungua Application yoyote ile kwa kupokea SMS kwenye simu yako, Kumbuka hii ni sehemu ndogo tu ya app hii na kupitia video hii ningependa ujue app hii ambayo ukweli inafanyakazi kubwa sana ya kufanya simu yako iendelee kuwa Smartphone.

Kama umefuatilia video yote hadi mwisho basi hakikisha unapakua app iliyotajwa hapo juu kupitia link HAPA, kama unataka kujua zaidi kuhusu app hii unaweza kutoa maoni hapo chini ili tutengeneze series ya video kuhusu app hii.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unajiunga nasi kwenye channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube, ili kuwa wa kwanza kupata maujanja mbalimbali.

Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine (Updated)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.