in

Sasa Fahamu ya Muhimu Kuhusu COVID-19 Kupitia WhatsApp

Pata maelezo kutoka WHO kupitia programu yako ya WhatsApp

Sasa Fahamu ya Muhimu Kuhusu COVID-19 Kupitia WhatsApp

WHO kwa kushirikiana na WhatsApp, kwa pamoja wamekuja na njia mpya ya kusambaza elimu kuhusu Virusi vya Corona au COVID-19 kwa watu mbalimbali duniani kote kupitia programu ya WhatsApp.

Kwa mujibu wa page ya Twitter ya WHO nchini Uganda, sasa utaweza kupata taarifa kuhusu virusi vya corona ikiwa pamoja na kuuliza maswali mbalimbali moja kwa moja kwenye programu ya WhatsApp. Ili kuweza kuwezesha sehemu hiyo unatakiwa kuwa na WhatsApp kisha ongeza namba ifuatayo +41 79 893 18 92 kwenye phonebook yako kisha refresh contact na moja kwa moja chat na namba hiyo kwa kujisajili kwa kuandika neno Join.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya hapo utaweza kupata taarifa za muhimu kupitia WhatsApp pale zitakapo toka rasmi, na pia utaweza kuuliza maswali pamoja na kusoma taarifa nyingine za muhimu kuhusu virusi vya corona au COVID-19.

Sasa Fahamu ya Muhimu Kuhusu COVID-19 Kupitia WhatsApp

Kama unavyoweza kuona hapa juu, hii ndio menu ambayo itaweza kutokea mara baada ya kuandika neno “Join”. Kupitia menu hiyo utaweza kujua yafuatayo.

  1. Latest number – kwa kuandika 1 kwenye sehemu ya kuchati utaweza keletewa takwimu za vifo kwa ujumla, na kesi mpya za virusi vya corona kwa muda wa masaa 24.
  2. Protect yourself – kwa kuandika 2 kwenye sehemu ya kuchati utaweza kueletewa maelezo ya muhimu ya jinsi ya kujilinda dhidi ya virusi vya corona pamoja na video zenye kuonyesha jinsi ya kujikinga.
  3. Your question answered – kwa kuandika namba 3 unaweza kupata maswali ambayo yanaulizwa zaidi kuhusu virusi vya corona ikiwa pamoja na majibu yake kwa ujumla, kupitia sehemu hii utaletewa swali na ili kupata jibu lake unatakiwa kuchagua namba ya swali kwa kuandika kwenye sehemu ya kuchat na moja kwa moja utaletewa jibu la swali hilo.
  4. Mythbusters – kwa kuandika namba 4 kwenye sehemu ya kuchati utaweza kuletewa maelezo ya muhimu ambayo huwenda ulisikia na ulidanganywa kuhusu virusi vya corona na hapo utapewa majibu sahihi tofauti na maelezo ambayo pengine ulidanganywa kwa namna moja ama nyingine.
  5. Travel advice – kwa kuandika namba 5 hapa utaweza kueletewa maelezo ya muhimu kuhusu ushauri wa jinsi ya kusafiri salama kama unasafiri kwa namna moja ama nyingine.
  6. News & Press – kwa kuandika namba 6 hapa utaletewa maelezo ya muhimu yanayotokana na habari mpya na taarifa mbalimbali kuhusu virusi vya corona.
  7. Share – kwa kuandika namba 7 kwenye sehemu ya kuchat utaweza kuletewa link maalum ambayo unaweza kutumia kushare na ndugu na jamaa waliopo kwenye whatsapp ambao unataka nao waweze kupata sehemu hii ambayo itawasaidia kupata maelezo ya muhimu kupitia WhatsApp.
  8. Donate – kwa kuchagua namba 8 utaweza kuchangia kupitia mfuko maalum utakao saidia kupambana dhidi ya corona. (sehemu hii ya kuchagia kwa Tanzania haifanyi kazi).

Hivyo ndivyo ambavyo unaweza kupata maelezo ya muhimu kuhusu virusi vya corona kupitia programu yako ya WhatsApp. Kumbuka maelezo yote hayo yanatoka kwenye tovuti ya WHO na unaweza kuyapata maelezo hayo kwa kutembelea tovuti hiyo moja kwa moja.

Kwa taarifa zinazohusu virusi vya corona kwa hapa Tanzania, hakikisha unatembelea tovuti ya wizara ya afya Tanzania hapa. Pia unaweza kusikiliza radio pamoja na kuangalia TV ili kupata taarifa sahihi kuhusu virusi vya corona.

Sasa Fahamu ya Muhimu Kuhusu COVID-19 Kupitia WhatsApp
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.