in

Hivi Karibuni Utaweza Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Utaweza kuonyesha matangazo kwenye video zako na kupata pesa

Hivi Karibuni Utaweza Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Baada ya Instagram kuondoa kitufe cha IGTV kwenye ukurasa wake wa Home, Habari za hivi karibuni zinasema matandao wa instagram upo kwenye hatua za awali za kuwezesha wabunifu wa video kuweza kutengeneza pesa kupitia sehemu ya IGTV kupitia mtandao huo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Techcrunch, sehemu hiyo inasemekana itakuwa inafanana na ile ya mtandao wa Facebook ambayo inaruhusu watumiaji kuweka matangazo katikati ya video na mmiliki halali wa video hupokea asilimia 55 ya kipato kinacho tokana na video hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa sasa bado hakuna taarifa ya kiasi cha mapato ambacho wamiliki wa video za IGTV watapokea, lakini kwa sababu Instagram hutumia mfumo mmoja wa matangazo na Facebook, huwenda kiwango hicho kikabaki kuwa asilimia 55 kama ilivyo kwenye Facebook Watch kwa sasa.

Hivi Karibuni Utaweza Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Kama unavyoweza kuona hapo juu, wapakiaji wa video kwenye sehemu ya IGTV watakuwa wanapitia uhakiki maalum ambao pale mtumiaji anapo thibitisha basi uruhusiwa kuonyesha matangazo kwenye video zake za IGTV. Awali inasemekana instagram ilikuwa ikiwalipa wasanii wakubwa kuweza kuweka video za matangazo kwenye kurasa zao za IGTV kupitia Instagram.

Kwa mujibu wa tweet kutoka kwa mmoja wa viongozi wakuu wa mtandao wa Instagram, amethibitsha kuwa instagram inafanyia kazi sehemu hiyo na ipo kwenye hatua za awali za kusaidia wabunifu wa video kupitia IGTV kuweza kutengeneza pesa kupitia video zao.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu sehemu hiyo, wala haija julikana ni sheria gani zitatumika kuweza kukubali video za IGTV kuwekewa matangazo. Inawezekana kabisa sheria hizo zikafanana kabisa na sheria za Facebook ambazo unaweza kuzisoma kwa urefu hapa. Kwa taarifa zaidi kuhusu kupata pesa kupitia IGTV hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech.

Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa "X"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.