in

Instagram Kuja na Reaction Kwenye Sehemu ya DM

Hivi karibuni utaweza kujibu meseji za DM kwa kutumia emoji za reaction

Instagram Kuja na Reaction Kwenye Sehemu ya DM

Mtandao wa instagram umekuwa ukifanya maboresho mbalimbali kila siku, hivi karibuni tegemea kuona maboresho mapya ambao sasa utakuwa unaweza kujibu DM au Instagram Direct Message kwa kutumia emoji za reaction.

Kwa mujibu wa tovuti ya Social Media Today, sehemu hiyo mpya itakuwa ndani ya ukurasa wa DM ambapo chini ya meseji uliyo tumiwa utaweza kuona sehemu mpya ya emoji za reaction ambazo zinafanana kabisa na zile zilizopo kwenye sehemu ya Facebook comment.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama unavyoweza kuona hapo juu, hivyo ndivyo itakavyokuwa kwenye ukurasa wa DM ambao sasa utaweza kujibu meseji ya mtu kwa kutumia reaction. Hata hivyo kwa mujibu wa Jane Manchun Wong @wongmjane ambaye ndiye aliyegundua sehemu hiyo kabla ya kutoka kwake, ameandika kwenye twitter kuwa sehemu hiyo inatarajia kuja hivi karibuni kwani meneja wa mawasiliano na teknolojia aliyemtaja kwa jina la @alexvoica ame thibitisha kuwa sehemu hiyo ipo kwenye majaribio.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi za lini sehemu hii itawafikia watumiaji wote. Hadi sasa inasemekana sehemu hii ipo kwenye hatua za awali za majaribio na bado haijafika kwenye programu za majaribio za Instagram.

Kupata taarifa pale sehemu hii itakapo wafikia watumiaji wote ikiwa pamoja na wewe hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment