in

Sunday Movie #1 : Movie Nzuri ya Teknolojia ya Kuangalia

Hii hapa movie nzuri ya teknolojia ya kungalia Jumapili ya leo

Sunday Movie #1 : Movie Nzuri ya Teknolojia ya Kuangalia

Karibu kwenye kipengele kipya cha Sunday Movie, kupitia kipengele hichi tutakuwa tukiangalia Movie nzuri ambayo unaweza kuangalia siku ya jumapili, Movie hizi zitakuwa ni movie zinazohusu teknolojia hivyo kama wewe ni mpenzi wa Movie na pia ni mpenzi wa teknolojia basi natumaini utaweza kufurahia kipengele hichi. Lakini neno langu sio sheria ni vyema tujue maoni yako je unaonaje kipengele hichi.. maoni yako hapo chini.

Sunday Movie #1 – Countdown

Kwa siku ya leo jumapili hii tuanze na movie hii ya Countdown, Movie hii inamuhusu muuguzi ambae anapakua programu inayoitwa Countdown ambayo inadai kutabiri wakati mtu atakufa, programu hiyo inamwambia muunguzi huyo kuwa ana siku tatu za kuishi. Wakati muda wake wa siku tatu ukiendelea kuisha, muunguzi huyo anatafuta njia ya kuokoa maisha yake kabla ya wakati wake kumalizika.

Mafunzo ya Movie Hii

Movie hii imechanganya teknolojia pamoja na maswala ya imani na kwa pamoja inatoa mafundisho mengi sana hasa kwenye ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia. Fundisho kubwa kwenye Movie hii ni watumiaji wa teknolojia kuwa makini sana kusoma vigezo na masharti ya programu wanazotumia kwenye simu zao kabla ya kutumia.

Ni wazi kuwa wengi wetu hatuna muda kabisa wa kusoma vigezo na masharti kwenye programu tunazo install kwenye vifaa vyetu, wengi wetu hubonyeza kwa haraka “I agree na kuanza kutumia programu bila kujua ni masharti gani yameandikwa. Movie hii inaonyesha kuwa ni muhimu kusoma vigezo na masharti ya utumiaji kabla ya kutumia programu yoyote kwenye kifaa chochote.

Download Hapa

Unaweza kupata Movie hii moja kwa moja kwenye kifaa chako chochote kwa kudownload kupitia link hapo chini, Link hii ya sasa ni link ya moja kwa moja hivyo huna haja ya kufanya chochote zaidi ya kubofya hapo chini na kupakua Movie hii moja kwa moja.

Download Movie Hapa

Amani Joseph

Sunday Movie #1 : Movie Nzuri ya Teknolojia ya Kuangalia

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment