in

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Sticker Zinazotembea

Stika hizo zitakuja kwa makundi kama zilivyo stika zilizopo sasa

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Sticker Zinazotembea

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu ya WhatsApp basi hivi karibuni tegemea kuona aina mpya ya stika ambazo zitakua zinatembea. Kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, WhatsApp inategemea kuja na aina hiyo ya sticker ambazo zitakuwa zinafanana kabisa na sticker zilizopo sasa lakini tofauti yake kubwa hizo zitakuwa zikitembea (Animated).

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Sticker Zinazotembea

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Stika hizo zinasemekana kuwa kwenye vikundi mbalimbali na utaweza kupakua stika hizo kutoka kwenye app nyingine tofauti au kutumia stika ambazo zitakua zinakuja na programu ya WhatsApp. Unaweza kuangalia video hapo chini kuona jinsi stika hizo zitakavyokuwa zinafanya kazi.

Mbali na hayo, hivi karibuni inategemewa kuwa WhatsApp italeta muonekano wa Giza kwenye programu ya WhatsApp, muonekano ambao unasubiriwa na watu wengi kwa hamu ukitarajia programu hiyo inatumika na watu wengi zaidi kadri siku zinavyokwenda.

WhatsApp Kuja na Aina Mpya ya Sticker Zinazotembea

Kwa sasa kama unataka kujua jinsi ya kuweka sehemu ya Dark Mode kwenye app ya Instagram basi unaweza kufuata hatua kwa hatua hapa na utaweza kusaidia macho yako hasa wakati wa usiku kwa kuwasha sehemu hiyo mpya ya muonekano mweusi au Dark Mode.

Apps za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Simu Yako (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment