Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite

Toleo jipya la bei rahisi la simu ya Samsung Galaxy Note 10 ya 2019
Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite

Baada ya kuangalia sifa na bei za Samsung Galaxy S10 Lite, sasa twende moja kwa moja tukaangalie sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite. Kama ilivyo kwa S10, Simu hii pia ina-tofauti sana na simu ya Galaxy Note 10 ambayo imezinduliwa mwaka jana 2019.

Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja tukangalie sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite ambayo imezinduliwa hivi karibuni.

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite

Advertisement

Sifa za Samsung Galaxy Note 10 Lite

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Mongoose M3 & 4×1.7 GHz Cortex-A55)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9810 (10 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP18.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6 au GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12, f/1.7, 27mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 12, f/2.2, 12mm (ultrawide), kamera ya mwisho ni Megapixel 12, f/2.4, 1/5.0″, 1.12µm, dedicated macro camera. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi za Prism White, Prism Black, Prism Blue.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint (under display, optical), accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite

Bei ya Samsung Galaxy Note 10 Lite

Kwa upande wa bei, Samsung Galaxy Note 10 Lite inategemea kuingia sokoni mwezi wa pili au watatu kwa Tanzania na inategemewa kuuzwa kwa takribani shilingi za kitanzania TZS 1,550,000 bila kodi. Kwa mujibu wa Samsung simu hii bado bei yake haijatangazwa rasmi hivyo bei hiyo hapo juu inaweza kubadilika pale Samsung itakapo tangaza bei halisi ya simu hii. Soma hapa kujua zaidi kuhusu Galaxy Note 10 Lite.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use