Samsung Yatambulisha “Ballie” Roboti ya Kusaidia Nyumbani

Roboti hii inaweza kufanya mambo mbalimbali nyumbani kwako
Samsung Yatambulisha "Ballie" Roboti ya Kusaidia Nyumbani Samsung Yatambulisha "Ballie" Roboti ya Kusaidia Nyumbani

Kupitia mkutano wa CES 2020, Kampuni ya Samsung imetangaza bidhaa zake mbalimbali na kupitia makala hii hebu tuongelee kuhusu “Ballie”. Ballie ni roboti mpya kutoka Samsung ambayo imetengenezwa maalum kwaajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za nyumbani.

Kupitia mkutano huo uliofanyika huko Las Vegas nchini Marekani, Samsung imetangaza roboti hiyo ambayo inatumia mfumo wa AI kuweza kuunganisha vifaa mbalimbali ndani ya nyumba yako (smart devices) na kuweza kufanya kazi mbalimbali pale inapo hitajika.

https://www.youtube.com/watch?v=c7N5UDZX7TQ

Advertisement

Kwa upande wa upatikanaji, Samsung haikutangaza habari yoyote kuhusu wakati gani roboti hiyo ya Ballie itapatikana kwa wateja duniani, au itauzwa kwa kiasi gani. Kwa hivyo ni ngumu kujua kama haya ni maoni tu ya samsung kwenye siku zinazokuja au kama roboti hii ya “Ballie” itafanikiwa kutoka nje ya mkutano wa CES 2020 na kuwafikia watumiaji duniani kote.

Lakini kwa hivi sasa, endelea kuungana nasi tutakuletea habari zote zilizo jiri kwenye mkutano wa CES 2020, hakikisha unatembelea ukurasa wetu maalum kwaajili ya kupata habari zote zilizojiri kwenye mkutano huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use