in

Sasa Tumia Ulinzi wa Fingerprint Kwenye WhatsApp (Android)

Utaweza kuzuia mtu kusoma meseji zako kwa kutumia alama za vidole

Sasa Tumia Ulinzi wa Fingerprint Kwenye WhatsApp (Android)

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye sasa watumiaji wa Android wataweza kutumia ulinzi wa alama za vidole au Fingerprint kwenye programu ya WhatsApp. Sehemu hiyo inasaidia kufunga programu hiyo na kuiweka salama, bila kuruhusu mtu yoyote kufungua programu hiyo pamoja na ujumbe wowote unaoingia bila kuweka alama ya kidole.

Kwa sasa sehemu hiyo tayari inapatikana kwenye toleo jipya la WhatsApp na unaweza kuipata kupitia sehemu ya Settings > Account > Privacy Kisha shukua mpaka mwisho wa ukurasa huo utaona Sehemu ya Fingerprint lock.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa Tumia Ulinzi wa Fingerprint Kwenye WhatsApp (Android)

Baada ya kufika kwenye sehemu hiyo utakuta sehemu hiyo ya fingerprint imezimwa hivyo unatakiwa kuiwasha sehemu hiyo, unaweza kuchagua sehemu hiyo ianze kufanyakazi mara moja (immediately), baada ya dakika moja (After 1 minute), au baada ya nusu saa (After 30 minutes).

  • Utakapo chagua Immediately basi mara baada ya kioo cha simu yako kuzima sehemu hiyo itafunga programu yako mara moja.
  • Utakapo chagua After 1 minute hapo programu yako itahitaji fingerprint kama utakuwa hujatumia programu hiyo ndani ya dakika moja.
  • Utakapo chagua After 30 minute hapo programu yako itahitaji fingerprint kama utakuwa hujatumia programu hiyo ndani ya dakika 30 au nusu saa.
  • Pia kama ukizima sehemu ya Show content in notification (hii inakuwa imewashwa) hapo mtu hatoweza kuona meseji zako kwenye sehemu ya notification juu ya simu yako mpaka hapo utakapo weka alama ya kidole.

Kama kwa namna yoyote bado hujaona sehemu hii ya Fingerprint kwenye simu yako ya Android, basi hakikisha una sasisha (Update) programu yako ya WhatsApp kupitia soko la Play Store na moja kwa moja fungua kwenye ukurasa huo wa Security na utaweza kuona  sehemu hiyo. Unaweza kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa wa programu ya WhatsApp moja kwa moja.

WhatsApp Messenger
Price: Free

Kama kuna sehemu yoyote utakuwa umekwama usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutajitahidi kukusaidia mara moja. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Apps Nzuri Kwaajili ya Kupakua Video za Aina Yoyote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

5 Comments