in

Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kupitia Wapepa App

App mpya kwaajili ya kubadilisha muonekano wa simu yako ya Android

Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kupitia Wapepa App

Ni kweli kwamba tunapo chukua uamuzi wa kununua simu mpya tunakuwa tumepanga kudumu na simu hizo kwa muda mrefu, lakini wote tunajua uhusiano wa muda mrefu unafika mahali unaona kama kile ulichonacho ni kitu cha kawaida na hii inasababishwa na kuzoea kitu hicho kutokana na kuto kubadilika kwa muda mrefu.

Sababu hii ndio imefanya kuwaletea Wapepa App, Hii ni app mpya kabisa ya wallpepa ambayo inakupa uwezo wa kupakua wallpaper nzuri na kuziweka moja kwa moja kwenye simu yako. Ukweli ni kwamba app hii ina uwezo mkubwa sana wa kubadilisha muonekano wa simu yako kwa asilimia kubwa na kufanya uone simu yako mpya.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kupitia Wapepa App

Jinsi ya kutumia app hii ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kupakua app hii kisha moja kwa moja chagua wallpaper unayo ipenda kisha bofya kitufe cha Apply na moja kwa moja chagua sehemu unayotaka kuweka wallpaper hiyo, kama ni kwenye Home Screen, Lock Screen au Home na Lock Screen. Pia unaweza ku-edt wallpaper kwa kubofya kitufe cha edit, bila kusahau sehemu ya kutoa maoni ambao unaweza kutoa maoni juu ya wallpaper husika.

App hii ni rahisi sana kutumia na tutakuwa tunaweka wallpepar mpya kila siku ili kuhakikisha huchoki simu yako kwa namna yoyote ile, unaweza kujaribu app hii kwa kupakua kupitia link hapo chini.

WAPEPA - Wallpaper
Price: Free+
Badilisha Muonekano wa Simu Yako Kupitia Wapepa App
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.