in

Jiandae na Samsung Galaxy M20s Simu Yenye Battery ya 6000 mAh

Simu yenye battery kubwa kuliko simu zote za Samsung zilizotoka hadi sasa 2019

Jiandae na Samsung Galaxy M20s Simu Yenye Battery ya 6000 mAh

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi za ujio wa simu mpya ya Samsung Galaxy M, simu ambayo inasemekana kuwa na battery kubwa zaidi kuliko simu zote za Samsung zilizotoka hadi sasa mwezi wa nane mwaka huu 2019.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya GSMArena, inasemekana simu hiyo itakuwa ni toleo la maboresho la simu ya Galaxy M20 simu ambayo ilizinduliwa mapema mwaka huu. Galaxy M20s ndio jina la simu hiyo mpya ambayo inasemekana kuja na battery kubwa ya 6000 mAh, battery ambayo ni karibia mara mbili ya battery ya simu Galaxy Note 10 pamoja na Galaxy S10.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Jiandae na Samsung Galaxy M20s Simu Yenye Battery ya 6000 mAh

Mpaka sasa toleo la Galaxy M20 linakuja na battery ya 5000 mAh ambayo ukweli inaweza kudumu na chaji hadi siku mbili kutoka na matumizi yako. Binafsi nimefanikiwa kutumia simu hii na ukweli inaweza kudumu na chaji kwa muda mrefu sana.

Jiandae na Samsung Galaxy M20s Simu Yenye Battery ya 6000 mAh

Hata hivyo kwa sasa hakuna ripoti zaidi kuhusu simu hii mpya zaidi ya ukubwa wa battery yake, hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu sifa kamili za simu hii pamoja na bei yake, bila kusahau mahali unapo weza kununua simu hii kwa bei nafuu. Kwa sasa unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili pamoja na bei ya toleo la sasa la Galaxy M20.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.