in

Fahamu App Mpya ya KLIK LOKO, Uza na Nunua Vifaa vya Kielektroniki

Uza au nunua vifaa vya kielektoniki kwa haraka zaidi Tanzania

Fahamu App Mpya ya KLIK LOKO, Uza na Nunua Vifaa vya Kielektroniki

Kama wewe ni mpenzi wa maswala ya teknolojia basi ni wazi kuwa lazima utakuwa unapenda pia vifaa mbalimbali vya kielektroniki. Mbali na hayo ni wazi kuwa kwa hapa kwetu Tanzania kuna uhaba mkubwa wa mahali ambapo unaweza kununua na kuuza vifaa hivyo kwani mitandao mingine yenyewe imeangalia zaidi kuuza na kununua vitu zaidi mbalimbali zaidi ya elektroniki.

Ndio maana leo hii tunatambulisha kwenu KLIK LOKO, Hii ni app mpya kabisa ya mfumo wa Android ambayo inakuruhusu kuuza na kununua vifaa vya kielektroniki pekee. Kama wewe unayo simu ambayo unataka kuuza au kama unayo laptop au vifaa vingine vya kielektroniki basi app hii itakusaidia sana kufanya hivyo kupata wateja.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Fahamu App Mpya ya KLIK LOKO, Uza na Nunua Vifaa vya Kielektroniki

Mbali ya kuuza pia utaweza kununua bidhaa mbalimbali za kielektroniki kwa urahisi na haraka. Sababu za kuja na programu hii ni kukupa sehemu pekee wewe mwana teknolojia, ambayo itakusaidia kuuza au kununua kitu chochote cha elektroniki kwa haraka tofauti na mitandao mingine. Baadhi ya mambo yaliyomo ndani ya app ya KLIK LOKO ni pamoja na

  • Kupitia App hii utaweza kupata ofa ya matangazo ya bure ya kulipia pale unapo jisajili.
  • Utaweza kuchat moja kwa moja kupitia App na mteja mwenye kifaa.
  • Utaweza kuweka Matangazo bila kikomo.
  • Utapata ujumbe moja kwa moja kama mtu atapenda kifaa chako.
  • Utaweza kuweka Picha Zaidi ya 4 kwa Haraka.
  • Utaweza kulipia matangazo kwa kutumia Salio la kawaida kwa mitandao ya (Vodacom na Tigo) kupitia Google.
  • Na mengine mengi…..

Kwa sasa toleo la kwanza la App ya KLIK LOKO tayari linapatikana kupitia soko la Play Store, kama unatumia simu ya Android hebu basi tujumuike wote kujaribu app hii pengine inaweza kuwa suluhisho la kununua au kuuza bidhaa za kielektroniki kwa haraka hapa nchini Tanzania.

Kwa kuwa hili ni toleo la kwanza naimani tumejitahidi kadri iwezekanavyo kutengeneza app bora, lakini hakuna kizuri kisicho na kasoro hivyo ningependa kupata maoni yako umeonaje app hii.. unaweza kutoa maoni yako hapa au kupitia soko la Play Store mara baada ya kutoa nyota unazodhani app hii inastahili. Tuko pamoja na tunaendelea kusubiri maoni yako.

Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

6 Comments