in

Simu za Huawei Kuzuiwa Kuja na Facebook, Instagram na WhatsApp

Simu mpya za Huawei hazitokuja na apps za Facebook, Instagram pamoja na WhatsApp

Simu za Huawei Kuzuiwa Kuja na Facebook, Instagram na WhatsApp

Baada ya kampuni ya Huawei kuzuiwa kufanya biashara na kampuni za marekani, mambo bado yanaendelea kuwa mabaya kwa kampuni hiyo baada ya hivi karibuni kampuni ya Facebook kuzuia simu za huawei kuja na apps za Facebook, Instagram pamoja na WhatsApp.

Kwa mujibu wa tovuti ya Reuters, Facebook imepiga marufuku simu mpya za Huawei kuja na programu za Facebook zikiwa ndani ya simu hizo moja kwa moja. Yaani pale mteja anapo nunua simu mpya za Huawei hatoweza kukuta programu za Facebook, Instagram na WhatsApp kama inavyokuwa kwenye simu nyingi za Android.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo, simu zote za Huawei ambazo zipo sokoni kwa sasa zitaendelea kutumia programu hizi hadi hapo huduma za Google zitakapo sitishwa kwenye simu hizo. Aidha simu zote mpya ambazo zitakuwa zinatoka kuanzia sasa zitakuwa hazina kabisa programu hizo na inawezekana ikawa ni ngumu sana ku-install programu hizo kwenye simu hizo.

Kwa sasa inasemekana kuwa, Huawei inashulikia mfumo wake mpya wa uendeshaji ambao unasemekana kuwa tayari na utaweza kuanza kutumika kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019, inasemekana mfumo huo utakuwa na uwezo wa kuruhusu mtumiaji ku-install apps mbalimbali za mfumo wa Android.

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili kama apps za Instagram, Facebook na WhatsApp zita simama kufanya kazi kwa ujumla, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa zaidi pindi tutakapo zipata.

Amani Joseph

Simu za Huawei Kuzuiwa Kuja na Facebook, Instagram na WhatsApp

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Mfumo wa iOS 17 Kupatikana Rasmi September 18 (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.