Tigo Tanzania Yazindua Huduma kwa Wateja Kupitia WhatsApp

Sasa utaweza kupata ufumbuzi wa matatizo kwa kupitia WhatsApp
Tigo Tanzania Yazindua Huduma kwa Wateja Kupitia WhatsApp Tigo Tanzania Yazindua Huduma kwa Wateja Kupitia WhatsApp

Baada ya kampuni ya MTN ya nchini Afrika ya kusini kuanzisha huduma ya kununua salio kwa kutumia WhatsApp, hivi karibuni kampuni ya kutoa huduma za simu ya Tigo Tanzania nayo imekuja na huduma inayo fanana na hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Bi Mwangaza matotola ambaye ni mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Tigo Tanzania, amesema huduma hiyo mpya itawasaidia wateja wake kuweza kuwasiliana na watoa huduma kwa urahisi na kupewa msaada wa utatuzi wa matatizo mbalimbali moja kwa moja kwa kupitia programu ya WhatsApp.

Hata hivyo wateja wataweza kupewa majibu ya papo kwa papo pale wanapotuma ujumbe wa WhatsApp kupitia namba 0675100100.

Advertisement

Tofauti na huduma ya MTN ambayo hutumia teknolojia ya WhatsApp Bot au WhatsApp Business API, huduma hii mpya ya Tigo yenyewe itakuwezesha kuwasiliana na watoa huduma moja kwa moja na sio roboti kama ilivyo zoeleka kwenye huduma nyingi kama hizi.

Kwa sasa huduma hii tayari inapatikana kwa watumiaji wa Tigo na unaweza kuwasiliana na watoa huduma wa Tigo kupitia WhatsApp kwa kuhakikisha una save namba hiyo hapo juu kisha tuma ujumbe kuweza kupata msaada wa huduma za Tigo Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use