in

Mwanzo au Mwisho wa Simu Mpya za Samsung Galaxy Fold

Huenda huu ukawa ndio mwisho wa simu za Galaxy Fold

Mwanzo au Mwisho wa Simu Mpya za Samsung Galaxy Fold

Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya teknolojia basi lazima utakuwa unajua kuhusu simu mpya ya Samsung Galaxy Fold, simu hii ni ya kwanza kabisa kutoka Samsung yenye mtindo wa kisasa wa kujikunja katika ya kioo.

Lakini kama umewahi kuisikia simu hii, basi lazima utakuwa unajua kuwa siku za karibuni simu hizi zilionekana kuwa na matatizo ya kioo siku chache kabla ya kuanza kuingia sokoni. Baadhi ya watumiaji wa kwanza wa simu hizo ambao walikuwa ni waandishi wa habari, walipata kugundua matatizo hayo baada ya vioo vya simu hiyo kuanza kuonekana kuwa na matatizo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mwanzo au Mwisho wa Simu Mpya za Samsung Galaxy Fold

Matatizo hayo yali sababishwa na aina ya kioo ambacho Samsung walitumia kwenye simu hii kwani kime-tengenezwa kwa plastiki ambayo kwa juu kinayo plastiki nyingine inayo onekana kama screen protector hivyo ni rahisi mtu kubandua plastiki hiyo kwa kudhani ni screen protector.

Mwanzo au Mwisho wa Simu Mpya za Samsung Galaxy Fold

Sasa kutokana na matatizo hayo siku za karibuni Samsung ilitangaza kubadilisha tarehe ya kuingiza simu hiyo sokoni ambapo awali ilikuwa imetangazwa simu hiyo itangia sokoni tarehe leo tarehe (26-04-2019). Hata hivyo mpaka sasa Samsung bado haija tangaza tarehe nyingine ya kuzindua au kuleta simu hiyo sokoni. Lakini kama haitoshi hivi karibuni Samsung imetangaza kuwataka wote walio nunua simu hizo kurudisha simu hizo haraka iwezekanavyo.

Wengi wa watumiaji hao ni waandishi wa habari ambao awali walipewa simu hiyo ili kufanyia mapitio (review) kabla simu hiyo haijaingia sokoni rasmi. Sasa kutokana na hili wengi wa waandishi hao wanasema kuwa huenda huu ndio ukawa mwisho wa simu hiyo ya Galaxy Fold ingawa kupitia tovuti ya GSMArena Samsung imesisitiza kuwa haijasitisha simu hiyo ila imepanga kufanya marekebisho ya simu hiyo yatakayofanya simu hiyo kuwa bora zaidi.

Mwanzo au Mwisho wa Simu Mpya za Samsung Galaxy FoldHata hivyo baada ya Samsung kutangaza hilo, imeanza kuonekana kuwa huenda simu hiyo ikasitishwa kabisa kutokana na Samsung kuto tangaza tarehe nyingine ya simu hizo kurudi sokoni, inawezekana kabisa samsung imegundua tatizo kwenye vioo vya simu hizo na pengine ndio sababu ya kuwataka watu wote kurudisha simu hizo kabla tatizo hilo halijajulikana kwa mara nyingine tena.

Lakini pia kwa upande mwingine inawezekana huu ndio ukawa mwanzo wa simu hii bora kutoka Samsung ambayo inakuja na teknolojia ya kisasa kwa mwaka huu 2019. Je wewe unaonaje kuhusu hili unadhani huu ni mwanza au mwisho wa Galaxy Fold..? tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.