in

Sasa Utaweza Kupeleka Mbele Video Kupitia Mtandao wa Instagram

Utaweza kusogeza mbele video zile za dakika moja

Sasa Utaweza Kupeleka Mbele Video Kupitia Mtandao wa Instagram

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram basi ni wazi unajua kuwa tofauti na video za IGTV au zile za Stories kupitia mtandao wa Instagram huwezi kusogeza mbele video hasa zile za dakika moja zinazo postiwa pamoja na picha kwenye profile mbalimbali.

Sasa hivi karibuni Instagram inategemea kubadilisha hayo kwa kuweka sehemu maalum ya kuweza kusogeza video hizo mbele, sehemu ambayo inafahamika kwa jina la (seekbar). Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa kwenye mtandao wa Android Police, sehemu hiyo kwa sasa ipo kwenye majaribio na inategemewa kuja hivi karibuni kwenye programu zote za Instagram.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama inavyo kuwa kwenye mtandao wa YouTube, mtumiaji wa instagram pia ataweza kusogeza video mbele kwa kugusa na kusogeza mtari unaopita kwa juu ya video inapocheza. Hata hivyo kupitia sehemu hiyo watumiaji wataweza pia kurudisha nyuma video moja kwa moja kupitia sehemu hiyo bila kusubiri video kuisha na kujirudia kama ilivyo sasa.

Mbali na hayo, Instagram tayari imesha fanya mabadiliko ya baadhi ya sehemu mbalimbali kwenye programu yake ya Android, kujua zaidi kuhusu sehemu hizo unaweza kusoma hapa . Tofauti na hayo kama unataka kujua lini sehemu hii mpya ya kusogeza video mbele itakuja kwenye programu zote za Instagram hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Amani Joseph

Sasa Utaweza Kupeleka Mbele Video Kupitia Mtandao wa Instagram

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Mfumo wa iOS 17 Kupatikana Rasmi September 18 (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.