in

MTN Yaanzisha Huduma ya Kununua Salio Kupitia WhatsApp

Sasa wateja wa MTN Afrika ya kusini wataweza kununu salio kwa haraka

MTN Yaanzisha Huduma ya Kununua Salio Kupitia WhatsApp

Mtandao mkubwa Afrika unaotoa huduma za simu MTN, umekuja na huduma mpya itakayo wawezesha wateja wake kununua muda wa maongezi pamoja na kufanya mambo mbalimbali kupitia programu ya WhatsApp.

Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, MTN imeanzisha huduma hiyo ambayo tayari imeshaanza kufanya kazi ya kuhudumia wateja wa mtandao huo wa nchini Afrika ya kusini. Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile kununua na kuangalia salio, kununua vifurushi vya data, kuangalia na kuendesha baadhi ya taarifa za kibenki pamoja na mambo mengine mengi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Ili kufanikisha kutoa huduma hizo zote, Kampuni ya MTN imetengeneza roboti ya kuchat WhatsApp au (WhatsApp Bot) ambayo hii hutumika kuunganisha kati ya mteja na mtandao huo kupitia programu ya WhatsApp, mteja ataweza kununua salio au kupata huduma nyingine kwa kuanza kuchat na roboti hiyo kama anavyochat kawaida kwenye programu ya WhatsApp.

MTN Yaanzisha Huduma ya Kununua Salio Kupitia WhatsApp

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu hakuna tofauti kati ya kuchat na mtu wa kawaida na kuchat na roboti ya kuchat WhatsApp, bali  kwa upande wa kuchat na roboti hiyo utaweza kujibiwa meseji kwa haraka zaidi. Ili mtumiaji kuweza kununua salio kwa kutumia WhatsApp anatakiwa kuweka taarifa zake za benki kama vile kadi namba, CVC na taarifa nyingine na moja kwa moja mtumiaji ataweza kununua salio kupitia akaunti hiyo kila atakapo tumia huduma hiyo.

Hata hivyo inasemekana kampuni ya MTN imetumia kampuni nyingine ya nchini Afrika ya kusini inayoitwa Clickatell ambayo ina ushirikiano na WhatsApp ambayo ndio iliyo tengeneza na kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wa MTN.

Kwa sasa WhatsApp inatoa huduma kama hii ya kuunganisha mtandao wa WhatsApp Business na wateja mbalimbali kupitia roboti za kuchat au WhatsApp Bots, lakini kwa sasa huduma hiyo ipo kwenye hatua za majaribio na ili kuweza kupata huduma hiyo kampuni yako inatakiwa kufuata vigezo na masharti ya utumiaji ikiwa pamoja na kuzingatia ukubwa wa kampuni husika.

Kama kampuni yako ni ya kiwango cha kati au ni kampuni kubwa na utaka kupata huduma kama hii ya WhatsApp Bots, unaweza kujiunga kupitia hapa pia maelezo zaidi yanapatikana kwenye ukurasa huu hapa.

MTN Yaanzisha Huduma ya Kununua Salio Kupitia WhatsApp
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.