in

Simu za Samsung Zitakazo Pata Mfumo wa Android 9 (Pie)

Hizi hapa ni baadhi ya simu Samsung zinazotarajiwa kupata Android 9 (Pie)

Simu za Samsung Zitakazo Pata Mfumo wa Android 9 (Pie)

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi ni wazi kuwa unatamani simu yako ipate mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie) na kwa kuwa tayari Google imeanza kufanya majaribio ya mfumo mpya wa Android Q, basi ni wazi kuwa tayari simu nyingi zimeanza kupokea mfumo huu wa Android 9.0.

Kwa leo ningependa kujulisha list fupi ya simu za Samsung ambazo zinatarajiwa kupata mfumo huu wa Android Pie, kama unatumia simu ya Samsung na ulikuwa unasubiria simu yako ipate mfumo mpya wa Android basi ni wakati wako kuangalia list hii kama simu yako itapata mfumo huu mpya.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Kumbuka kama unatumia simu za Galaxy S na Galaxy Note basi una haja ya kuangalia list hii kwani Samsung imesha tangaza kuwa simu zake hizo zitapata matoleo mapya ya mfumo wa Android 9.0 (Pie), mfumo ambao pia utakuja na muonekano mpya wa Samsung One UI. Pia ni vyema kujua kuwa simu za Galaxy S na Note ni zile ambazo sio za siku nyingi sana au zile ambazo tayari zina mfumo wa Android 8.1 (Oreo).

Baada ya kusema hayo sasa twende tukangalie list hii ya simu ambazo zinasemekana kupata mfumo huu mpya wa Android 9 (Pie).

Simu za Samsung Ambazo Tayari zina Android 9.0 (Pie)

 • Samsung Galaxy S9
 • Samsung Galaxy S9 Plus
 • Samsung Galaxy Note 9
 • Samsung Galaxy S8
 • Samsung Galaxy S8 Plus

Simu za Samsung Ambazo Zitapata Android 9.0 (Pie)

 • Samsung Galaxy Note 8
 • Samsung Galaxy A6 Plus (March)
 • Samsung Galaxy A6 (April)
 • Samsung Galaxy A7 2018 (April)
 • Samsung Galaxy A8 2018 (April)
 • Samsung Galaxy A9 2018 (April)
 • Samsung Galaxy J2 Core (April)
 • Samsung Galaxy J4 (April)
 • Samsung Galaxy J6 Plus (April)
 • Samsung Galaxy J7 Prime2 (April)
 • Samsung Galaxy J8 (April)
 • Samsung Galaxy On7 Prime (April)
 • Samsung Galaxy J4 Plus (May)
 • Samsung Galaxy J6 (May)
 • Samsung Galaxy A8 Star (June)
 • Samsung Galaxy J7 Neo (June)
 • Samsung Galaxy J7 Pro (June)
 • Samsung Galaxy J7 Duo (July)
 • Samsung Galaxy J7 (July)
 • Samsung Galaxy M10 (August)
 • Samsung Galaxy M20 (August)
 • Samsung Galaxy Xcover 4 (August)
 • Samsung Galaxy J3 2017 (September)

Simu za Samsung Zinazo tarajiwa Kupata Android 9.0 (Pie)

 • Samsung Galaxy S8 Active
 • Samsung Galaxy Note FE

Kwa sasa hizi ndio simu za Samsung zinazo semekana kupata mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie), hata hivyo simu nyingi za Samsung zitakazo pata mfumo huu pia kuna uwezekano wa simu hizo kupata muonekano mpya ya One UI. Kama simu yako haipo kwenye list hii basi usiwe na wasiwasi tutakuwa tuna update ukurasa huu kila mara tutakapo pata taarifa za simu nyingine za samsung zitakazo pata mfumo huo mpya wa Android 9.0 (Pie).

Amani Joseph

Simu za Samsung Zitakazo Pata Mfumo wa Android 9 (Pie)

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Mfumo wa iOS 17 Kupatikana Rasmi September 18 (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments