Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Huduma kubwa kuliko zote ni huduma mpya ya Apple TV+
Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Kampuni ya Apple hapo jana ilifanya mkutano wake ambao ulikuwa wa tofauti kidogo, mkutano huo ulikuwa sio kwa ajili ya kutangaza bidhaa za kielektroniki kutoka Apple, bali ulikuwa ni mkutano wa tofauti kwani Apple ilitangaza huduma zake mpya mbalimbali ikiwa pamoja na maboresho ya huduma za zamani.

Sasa kama hukuweza kufuatilia mkutano huu hapo jana leo nitaenda kukujulisha yote yaliyojiri kwenye mkutano huo ikiwa pamoja na huduma zote mpya zilizotangazwa kwenye mkutano huo. Basi bila kupoteza muda let’s get to it.

Apple News Plus (Apple News+)

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Advertisement

Tukianza na huduma mpya ya Apple News Plus, hii ni huduma mpya kabisa kutoka apple ambayo itakuwa inakupa nafasi ya kuweza kusoma majarida mbalimbali ambayo utaweza kuyasoma moja kwa moja kupitia simu yako ya iPhone, iPad pamoja na kompyuta yako ya Mac.

Kwa mujibu wa Apple, huduma hii inakuja na majarida zaidi ya 300 huku ikikupa uwezo wa kushare majarida hayo na familia kupitia vifaa vya Apple. Mbali na hayo huduma hii mpya ya Apple News Plus inakuja na habari pamoja na makala kutoka tovuti mbalimbali, huduma hii ya Apple news plus inapatikana kuanzia siku jana kupitia mfumo mpya wa iOS na MacOS, unachotakiwa kufanya ni kusasisha mfumo huo kwenye kifaa chako kisha washa app ya Apple News.

Jinsi ya Kutumia Apple News Plus ukiwa Tanzania

Huduma ya Apple News+ kwa Tanzania haipatikani lakini unaweza kutumia maujanja ili kuweza kupata huduma hii kwenye kifaa chako cha Apple. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua kifaa chako kisha bofya sehemu ya Settings > General > Language & Region kisha chagua kati ya nchi hizi United States, United Kingdom, au Australia, kisha baada ya hapo bofya Done.

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Baada ya hapo jaribu sasa kudownload app ya Apple News kupitia kifaa chako kwa kubofya hapo chini, ili kupata Apple News+ hakikisha umesasiha (update) mfumo mpya wa iOS kwenye simu yako kabla ya kufanya hatua hizi na hapo utaweza kupakua app hiyo kwenye kifaa chako moja kwa moja.

‎Apple News
Price: Free+

Apple Card

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Huduma nyingine mpya ambayo imezinduliwa hapo jana na kampuni ya Apple ni pamoja na huduma ya Apple Card. Hii ni aina mpya ya card ya kidigitali ambayo inatolewa na kampuni ya Apple. Kupitia app ya Wallet kwenye simu yako ya iPhone utaweza kujisajili na utapata kadi hii ndani ya dakika chache tu, kadi hii inaweza kutumika kufanya malipo dunia nzima pamoja na kufanya malipo kwa kutumia Apple Pay.

Mbali na hayo, kupitia app ya Wallet utaweza kuona matumizi yako uliyofanya kwa kutumia Apple Card na pia utaweza kuona sehemu nyingine mbalimbali kama vile tovuti au kwenye sehemu ulizo tumia pesa pamoja na baadhi ya huduma ulizo jiunga kwa kutumia malipo ya Apple Card. Pia utaweza kuona matumizi yako ndani ya wiki nzima yakiwa yamepangwa kwenye graph ili kusaidia kujua matumizi yako kwa ujumla.

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Kwa sasa bado hakuna taarifa kama kwa Tanzania tunaweza kutengeneza kadi hii ila endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa zaidi kuhusu kadi hii pamoja na njia za kujiunga kama itakuwa inawezekana kwa Tanzania.

Apple Arcade

https://www.youtube.com/watch?v=95FuVib8mcY

Kama wewe ni mpenzi wa Game basi Apple Arcade ni huduma mpya ya Apple kwa ajili yako, kupitia huduma hii utaweza kulipia kwa mwezi na utaweza kucheza game mbalimbali kupitia kifaa chako cha Apple TV, iPhone, iPad pamoja na Mac. Kwa mujibu wa Apple, huduma hii inakuja na games zaidi ya 100 na utaweza kucheza games hizo zote kwa kulipia moja tu kila mwezi.

Kizuri kuhusu huduma hii ni kuwa, utaweza kucheza game hizi bila kuwa na Internet baada ya kudownload na pia utaweza kuendelea kucheza kwenye kifaa chochote ikiwa vifaa vyako vyote vya apple vinatumia akaunti moja ya iCloud. Pia huduma hiyo itakuwa haina matangazo na pia itakuwa haina huduma za kununua vifurushi vya ndani ya game maarufu kama in-app purchases.

Apple Yaja na Huduma Mpya za Apple TV Plus, Apple Card na Nyingine

Huduma hii ya Apple Arcade inategemea kuanza kupatikana hivi karibuni kwenye nchi zaidi ya 150 kupitia kwenye ukurasa maalum ndani ya Apple Store. Kwa sasa bado hakuna taarifa kama Tanzania ni moja ya nchi hizo 150+ hivyo tutakupa taarifa pale tu tutakapo pata list nzima ya nchi zenye uwezo wa kutumia huduma hii mpya kutoka Apple.

Apple TV Plus (Apple TV+)

https://www.youtube.com/watch?v=Bt5k5Ix_wS8

Apple TV Plus ndio huduma mpya na kubwa iliyo tawala jana kwenye mkutano huu wa Apple, huduma hii ni kama Netflix na inakupa uwezo wa kuangalia filamu mpya mbalimbali pamoja na tamthilia kwa kulipia kwa kifurushi kila mwezi. Kama ilivyokuwa kwa upande wa Netflix, Apple pia itakuwa inatengeneza filamu na tamthilia ambazo zitakuwa zimegaramikiwa kwa asilimia 100 na kampuni ya Apple.

Kwa mujibu wa Apple, tayari kampuni hiyo imeshaungana na watengenezaji wakubwa wa filamu kama vile J.J Abrams, ambaye ametengeneza movie nyingi nzuri sana kama filamu zote za Mission: Impossible na filamu nyingine kama Star Wars na nyingine nyingi. Mbali na hayo huduma hiyo ya Apple TV+ inasemekana kuwa itakuwa haina matangazo na itakuwa inapatikana kwenye nchi zaidi ya 100. Kama ilivyo Netflix, utaweza kudownload filamu na thamthilia kwaajili ya kuangalia bila kutumia Internet.

Kwa sasa huduma hii nayo pia bado haijajulikana kama itakuja Tanzania, au kama Tanzania ni moja ndani ya nchi 100 zitakazo pata huduma hii mpya ya Apple TV+.

Na hizo ndio huduma zote mpya ambazo zimetangazwa na Apple kwenye mkutano wa hapo jana tarehe 25 March 2019. Kujua zaidi kuhusu huduma hizi pamoja na kujua yote mapya kwenye mfumo mpya wa iOS, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use