in

Samsung Galaxy S10 Plus Kuja na RAM GB 12 na ROM GB 1000

Inasemekana S10 Plus itakuwa na kamera tatu kwa nyuma na mbili kwa mbele

Simu za Samsung Galaxy S10 Plus

Hadi sasa zimebakia wiki kadhaa tu hadi kuzinduliwa rasmi kwa simu mpya za Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10+. Simu hizi zinategemewa kuja na muonekano mpya na teknolojia mpya tofauti kabisa na simu za mwaka jana (2018) za Galaxy S9 na Galaxy S9 Plus.

Sasa wakati tukiwa tunaendelea kuhesabu siku, hivi karibuni kumeibuka tetesi mpya kuhusu simu mpya ya Galaxy S10 Plus. Kwa mujibu wa mtandao wa GSMArena, inasemekana kuwa Galaxy S10 Plus itakuja na uwezo mkubwa wa RAM hadi GB 12 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya hadi TB 1, ambayo ni sawa na GB 1000. Mbali na hayo kwa mujibu wa tetesi hizo, Galaxy S10 Plus inasemekana itakuwa na kamera tatu kwa nyuma pamoja na kamera mbili kwa mbele tofauti na Galaxy S10 ambayo yenyewe itakuwa na kamera mbili kwa nyuma na kamera moja kwa mbele.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Galaxy S10 Plus (Tetesi)

Tetesi hizo pia zinaongeza kuwa, Galaxy S10 Plus itakuwa na kioo cha inch 6.4, kioo ambacho kinategemewa kuja na teknolojia ya Super AMOLED. Vilevile inasemekana kuwa mwaka huu Samsung itazindua simu za aina tatu za Galaxy S10 huku toleo la tatu likiwa la bei rahisi zaidi kuliko simu hizo za kawaida za Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus.

Galaxy S10 Plus (Tetesi) Pic 2

Vilevile inasemekana Galaxy S10 Plus itakuja ikiwa na rangi tatu za Black, White pamoja na Sea Green, huku simu zote zikitarajiwa kuja na mfumo mpya wa Samsung wa One UI, mfumo ambao unakuja na icon mpya na muonekano mpya kabisa kwenye simu za Samsung.

Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus zote zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 20 mwezi February na kupatikana rasmi tarehe 8 mwezi March mwaka huu 2019.

Kwa sasa hayo ndio machache kuhusu Galaxy S10 Plus, kujua zaidi endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech tutakujuza yote yatakayojiri kuhusu simu hizi mpya kutoka Samsung.

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.