in

Instagram Kuruhusu Kupost Mara Moja Kwenye Akaunti Zako Zote

Sasa utaweza kupost kwa urahisi kwenye akaunti zako zote

Instagram Kuruhusu Kupost Mara Moja Kwenye Akaunti Zako Zote

Mtandao wa Instagram unategemea kuleta mabadiliko mapya hivi karibuni, mabadiliko ambayo yatakuwa yanarahisha zaidi utumiaji wa mtandao huo, hasa kwa wale watu wenye akaunti zaidi ya moja za mtandao huo.

Kwa mujibu wa tovuti ya TechCrunch, sehemu hii mpya itaruhusu watumiaji wa instagram wenye akaunti zaidi ya moja, kuweza kupost post moja kwenye akaunti zao zote kwa mara moja bila kuingia kwenye akaunti hizo. Hapo awali, ili kupost post moja kwenye akaunti zako zote, ilikuwa ni lazima uingie kwenye akaunti hizo na kupost au ilikuwa ni lazima kutumia programu maalum za kupost kwenye mtandao huo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Lakini hivi karibuni mambo yatakuwa tofauti kwani kama unayo akaunti zaidi ya moja, utaweza kuona sehemu mpya wakati unapost, sehemu ambayo itakuwezesha kuchagua akaunti ambazo unataka post hiyo iweze kuonekana kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Instagram-Post-To-Multiple-Accounts

Kwa sasa inasemekana sehemu hii itaanza kuonekana kwa watu wenye simu za mfumo wa iOS na wiki kadhaa baadae itakuja kwa watumiaji wa mfumo wa Android.

Instagram imekuwa ikifanya mabadiliko mapya mara kwa mara, kama sehemu mpya ya Close Friend itakayo kuruhusu kushare Store na unao wajua, pamoja na sehemu mpya ya Voice Message ambayo itakusaidia kuweza kupost meseji za sauti kupitia DM. Mbali na hayo mabadiliko mengine inayotarajiwa kuja hivi karibuni ni aina mpya ya Profile ambayo itabadilisha kabisa muonekano wa profile yako kama inavyo onekana hapo chini.

Profile mpya Instagram

Nini maoni yako kuhusu muonekano huu pamoja na sehemu nyingine mpya kwenye mtandao wa Instagram, je sehemu hizi ni nzuri kwako au ?. Tuambaie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.