in

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Hizi hapa ndio mada zilizo tafutwa zaidi kupitia Tanzania Tech

mada za teknolojia 2018

Katika kuelekea mwisho wa mwaka 2018, leo Tanzania Tech tunakuletea mkusanyiko wa mada zilizosomwa sana hapa Tanzania Tech. Kupitia makala zaidi ya 1000 zilizopo hapa Tanzania Tech,  wasomaji wengi wameonekana kusoma mada hizi ambazo nyingi zimekuwa na maoni mengi pamoja na kuonekana kufurahiwa na wapenzi wengi wa teknolojia hapa Afrika mashariki.

10. Mada Kuhusu TV

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mwaka 2018 ulikuwa sio mwaka wa TV sana kwani kulikuwa hakuna habari nyingi sana kuhusu TV, pamoja na hayo hapa Tanzania Tech kulikuwa na muamko mkubwa wa watu mbalimbali kusoma makala mbalimbali zinazohusu TV. Moja ya makala zetu zinazohusu TV zime fanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 9k huku wangine wakionekana kutafuta zaidi kuhusu “TV Bora za kununua.

9. Kuhusu Simu za Infinix

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Kampuni ya Infinix imezindua simu nyingi kwa mwaka huu 2018, pia simu nyingi kutoka kampuni hii kwa mwaka 2018 zimekuja na muundo tofauti na wakisasa zaidi. Pia kampuni hii kwa mwaka 2018 imefanikiwa kuzindua simu yake ya kwanza yenye ukingo wa juu pamoja na simu yake ya kwanza yenye kutumia processor ya Snapdragon. Moja kati ya makala zetu zinazohusu simu za Infinix zimefanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 9.3k, huku watu wengi wakionekana kutafuta zaidi kuhusu Simu bora za Infinix.

8. Kuhusu Simu ya Tecno Camon X

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Simu ya Tecno Camon X ni moja kati ya simu mpya za tecno zilizo zinduliwa mwaka huu 2018, simu hii imeonekena kushika vichwa vya habari sana kwa mwaka 2018. Pengine labda Tecno Camon X ndio simu iliyo zungumziwa zaidi kwa mwaka 2018. Moja kati ya makala zetu zinazo zungumzia simu ya Tecno Camon X imefanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 9.8k, huku watu wengi wakionekana kutaka kujua zaidi kuhusu “Sifa za Tecno Camon X.

7. Mada Kuhusu Laptop

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Japo kuwa mwaka 2018 ulianza kwa laptop nyingi kuzinduliwa hasa kwenye mikutano ya teknolojia, lakini kuanzia kati kati ya mwaka laptop zimekuwa hazipo kwenye habari mbalimbali za teknolojia huku kampuni nyingine zikiwa zinazindua laptop kimya kimya bia hata kutoa taarifa. Moja kati ya makala zetu zinazohusu laptop zimefanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 10.6k, huku watu wengi wakionekana kutafuta zaidi Kuhusu laptop bora.

6. Kuhusu Kuflash Simu

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Ni wazi kuwa mwaka huu umekuwa ni mwaka wa smartphone, lakini pia ni kweli kuwa mwaka huu watu wengi wamepata matatizo mbalimbali ya simu na hii kupelekea watu wengi zaidi kusoma makala zinazohusu kuflash simu. Moja ya makala yetu inayohusu kuflash simu imesomwa na watu zaidi ya 10.7k, kuhu watu wengi wakitaka kujua Jinsi ya kuflash simu za Tecno.

5. Kuhusu Kutengeneza Apps

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Ukweli ni kuwa japo kuwa hivi sasa kuna website mbalimbali lakini ni wazi huko mbeleni itakuwa ni muhimu sana kwa kila website au tovuti kuwa na Application, pengine hii ndio sababu ya watu wengi zaidi kuonekana kusoma zaidi mada kuhusu utengenezaji wa Apps. Moja kati ya makala zetu zinazohusu utengenezaji wa apps imefanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 12k, huku watu wengi zaidi wakionekana kutafuta zaidi kuhusu Kutengeneza Apps za Android.

4. Kuhusu Nyimbo Mpya na Filamu

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Pamoja na kuwa tumajikita kwenye maswala ya teknolojia lakini ukweli ni kwamba na sisi pia tunapenda kusikiliza muziki pamoja na kuangalia filamu. Pia wasomaji wetu wanaonekana kufanya hivyo hivyo kwani moja ya makala yetu inayo husiana na nyimbo mpya na Filamu imefanikiwa kusomwa na watu zaidi ya 12.6k, huku watu wengi wakionekana kufafuta zaidi kuhusu Jinsi ya kudownload nyimbo mpya na Filamu.

3. Kuhusu Simu Bora za Kununua

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Hakuna mpinzani kwamba simu nyingi za aina tofauti zimetoka mwaka huu 2018, pengine ndio sababu ya watu wengi kuonekana wakisoma mada zinazohusu simu bora za kununua. Moja ya makala yetu ambayo inahusu simu bora za kununua imeonekana kusomwa na watu zaidi ya 16.2k, huku watu wengi zaidi wakionekana kutafuta zaidi kuhusu Simu bora za kununua.

2. Kuhusu Simu Bora za Samsung

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Samsung ni moja kati ya kampuni nyingi za simu zilizo zindua simu nyingi kwa mwaka 2018, Simu nyingi za samsung zimeonekana kupendwa na watu wengi sana pengine ndio sababu watu kusoma zaidi kuhusu makala za simu bora za Samsung. Moja ya makala yetu inayohusu simu bora za Samsung imesomwa na watu zaidi ya 17.3k, huku watu wengi zaidi wakionekana kufatuta kuhusu Simu bora za Samsung.

1. Kuhusu Simu Bora za Tecno

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018

Kama nilivyo kwambia awali mwaka 2018 ni mwaka wa Smartphone na ndivyo inavyoweza kuonekana kwa mada iliyosoma zaidi hapa Tanzania Tech. Simu za Tecno ni simu zinazo ongoza kwa mauzo hapa Afrika ndio maana watu wengi zaidi hapa Tanzania hutafuta zaidi kuhusu simu za Tecno. Moja kati ya makala zetu zinazohusu simu bora za Tecno zimesomwa na watu zaidi ya 54k, huku watu wengi zaidi wakionekana kutafuta zaidi kuhusu Simu bora za Tecno.

Na hizo ndio mada 10 ambazo zimeonekana kutafutwa zaidi hapa Tanzania Tech, ni wazi kuwa watu wana muitikio mkubwa kwenye maswala ya Teknolojia na ni furaha sana kwetu kuweza kuwepo hapa kwa ajili ya kuhudumia kiu za wasomaji wetu. Ukweli tunayo kila haki ya kutoa SHUKRANI KWA WASOMAJI WA TANZANIA TECH kwa kuweza kuwa nasi kuazia tulipo anza hadi sasa. Najua mnapoteza bando kila siku kusoma makala zetu, lakini naimani wote mnapata kile mnacho tafuta kwenye tovuti hii.

Tuna ahidi kuboresha huduma zetu zaidi na kuhakikisha kufikia watu wengi zaidi hapa Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla, tumeandaa huduma nyingi ambazo natumaini mtazifuhia pale zitakapo Tangazwa rasmi. Mwisho tunawatakia wote kwa ujumla HERI YA MWAKA MPYA 2019, MUNGU AWAJALIE MWAKA WENYE FURAHA NA MAFANIKO MENGI KWENYE KILA MTAKACHO KIFANYA. #Tukutane2019.

Mada 10 za Teknolojia Zilizosomwa Sana Mwaka 2018
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.