in

Yahoo Yaja na App Mpya ya Kuchat ya Yahoo Together App

Fahamu app mpya ya kuchat kwenye magroup ya Yahoo Together App

Yahoo Together app
Yahoo Together app

Kampuni ya Yahoo ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuja na huduma mpya ambayo itawaruhusu watumiaji wa huduma za Yahoo kuweza kuchat na ndugu na jamaa pamoja na marafiki kwa kutumia huduma mpya inayoitwa Yahoo Together.

Yahoo Together ni app ambayo imechukua muonekano na mtindo wa App ya Slack ambayo pia hutoa huduma ya kuchat kama ilivyo kwenye app hiyo mpya ya Yahoo Together. Tofauti na app ya Slack, App hii mpya ya Yahoo inakupa uwezo wa kuchat kwenye magroup lakini ni lazima kuwa na barua pepe ya mtandao wa Yahoo ndipo uweze kutumia app hiyo mpya.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Moja kati ya sehemu nzuri kwenye app hii ni sehemu inayoitwa Smart Reminders, sehemu hii itakuwezesha kuweka meseji ili ijitume yenyewe kwa wakati fulani na muda huo utakapo fika meseji hiyo itajituma kwa watu wote kwenye group husika. Sehemu nyingine ni Blast, highlights sehemu ambazo zitakupa uwezo wa kuwekea rangi kwenye meseji fulani ili watu wengine kwenye group waweze kuiona meseji husika pale watakapoingia kwenye group.

Kwa sasa tayari app hii ipo kwenye masoko ya Play Store na App Store hivyo unaweza kuipakua moja kwa moja kupitia masoko hayo kwa kubofya link yenye mfumo unaoendana na simu yako hapo chini.

  • Yahoo Together – Android
  • Yahoo Together – iOS

 

Yahoo Yaja na App Mpya ya Kuchat ya Yahoo Together App
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.