in

Apps #22 App Nzuri za Kusaidia Kutumia Instagram Kwa Urahisi

Jaribu app hizi nzuri za instagram kwenye simu yako ya Android

App za Instagram

Instagram ni moja kati ya mtandao unaotumiwa na watu wengi sana kwa sasa, pamoja na mtandao huo kuwa maarufu na muhimu kwa watumiaji mbalimbali siku hizi lakini bado watu wengi wanaonekana kushindwa kutumia mtandao huo kwa ukamilifu hivyo kushindwa kupata matokeo sahihi.

Ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea Apps nzuri za kuweza kukusaidia kutumia mtandao huo kwa urahisi zaidi na kwa haraka. App hizi ni maalumu kwa watumiaji wa Android na unaweza kuzipata bure kabisa kupitia soko la Play Store. Basi bila kupoteza muda twende tuangalie Apps hizi nzuri.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

1. InstaWho

InstaWho ni App nzuri kwaajili ya mtandao wa Instagram, app hii inakupa uwezo wa kujua ni nani anae angalia au alie angalia akaunti yako ya mtandao wa Instagram hivyo kukupa uwezo mzuri zaidi wa kujua nani ni mfuatiliaji mzuri wa akaunti yako na hivyo kukupa urahisi wa kuwasiliana nao.

2. insFull

InsFull ni appa nyingine nzuri sana ya Android kwaajili ya mtandao wa Instagram, App hii inakupa uwezo wa kuangalia profile picha ya mtu yoyote kwa haraka. App hii inauwezo wa kuonyesha picha hiyo kwa ukubwa kama picha nyingine kwenye mtandao huo wa Instagram.

3. Story Saver

Story Saver
Price: Free

Story Saver ni app nyingine inayokupa uwezo wa kutumia mtandao wa instagram kwa urahisi, App hii inakupa uwezo wa kudownload picha na video za Stories ambazo mara nyingi hizi huwa ni vigumu sana kuweza kuzipata.

4. Follower tracker for Instagram

App hii ni app nyingine kwaajili ya mtandao wa Instagram, App hii inakupa uwezo wa kujua mambo mbalimbali kuhusu akaunti yako. Kwa mfano unaweza kupata taarifa kuhusu watu mbalimbali ambao wameblock akaunti yako, mbali na hayo App hii inakupa mambo mengine mbalimbali kama kujua anaeangalia akaunti yako mara kwa mara pamoja na mambo mengine mbalimbali.

5. Analyzer for Instagram

App nyingine ambayo inafanana na app hiyo hapo juu ni app hii ya Analyzer for instagram, App hii inakupa uwezo mzuri na rahisi wa kuweza kujua mambo mbalimbali yanayohusu akaunti yako ya mtandao wa Instagram.

6. Repost Photo & Video for Instagram

App nyingine nzuri ambayo pengine ungependa kuitumia kwaajili ya mtandao wa Instagram ni App ya Repost, App hii inakupa uwezo wa ku-repost picha na video moja kwa moja kutoka kwenye Akaunti mbalimbali za mtandao wa Instagram.

Na hizo ndio app nzuri nilizo kuandalia kwa siku ya leo, Kama unataka kujua app nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Amani Joseph

Apps #22 App Nzuri za Kusaidia Kutumia Instagram Kwa Urahisi

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

OpenAI Mbioni Kuingiza Takribani Dola Bilioni 1 Kwa Miezi 12

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.