in

Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Poco F1 (Pocophone F1)

Kampuni ya Xiaomi imekuja na toleo la simu mpya za Poco

Sifa na bei ya Poco F1

Hivi karibuni kampuni ya Xiaomi ilitangaza kuzindua brand yake mpya ya simu ambayo itakuwa inaitwa pocophone. Hivi leo huko nchini india kampuni hiyo imefanikisha hayo kwa kuja na simu ya kwanza ambayo inatoka na jina hilo ambayo itakuwa inaitwa Poco F1.

Simu hii mpya kama zilivyo simu kutoka kampuni ya Xiaomi inakuja na muonekano mzuri sana pamoja na sifa nzuri huku ikiwa inauzwa kwa bei nafuu zaidi. Tukiangalia sifa za Pocophone F1 simu yenyewe inakuja na kioo cha Inch 6.18 kilicho tengenezwa kwa LCD ambacho kinakuja na teknolojia ya Full HD+ chenye resolution ya 2246 x 1080 pixels na uwiano au aspect ratio ya 18:7:9.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hii pia inakuja na processor ya Snapdragon 845 yenye uwezo wa CPU ya 2.8 GHz ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6 na GB 8, Simu hii pia inakuja kwa machaguo matatu ya ukubwa wa ndani kati ya GB 64, GB 128 pamoja na GB 256. Sifa nyingine za (Poco F1) Pocophone F1 ni kama zifuatazo.

Sifa za Poco F1 (Pocophone F1)

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2246 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~403 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64, GB 128 na nyingine GB 256 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 8 na nyingine ina RAM ya GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.0, 0.9µm yenye uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye ff/1.9, 1/2.55″, 1.4µm, dual pixel PDAF. Kamera nyingine inakuja na Megapixel 5 yenye f/2.0, 1.12µm, depth sensor. Zote zikiwa zinasaidiwa na Flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A (Quick Charge 3.0).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 2.0 ya Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Graphite Black, Steel Blue, Rosso Red na Armored Edition Kevlar.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Infrared face recognition, fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, barometer na compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face Unlock).

Bei ya Poco F1 (Pocophone F1)

Kuhusu bei simu hii itaanza kuuzwa nchini india kuanzia tarehe 29 mwezi huu wa nane, Kwa Rupee ya India INR20,999 ambayo ni sawa na Tsh 689,000 kwa toleo lenye GB 64 za ukubwa wa ndani. Toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 litauzwa kwa Rupee INR23,999 sawa na Tsh 789,000 huku toleo lenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 256 lenyewe litauzwa kwa Rupee INR 28,999 ambayo ni sawa na Tsh 950,000. Simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kwa nchi zingine kuanzia tarehe 27 ya mwezi huu.

Kumbuka Bei hizo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, hivyo bei inaweza kubadilika kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Amani Joseph

Xiaomi Yazindua Simu Mpya ya Poco F1 (Pocophone F1)

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.