in

Maujanja ya Jinsi ya Kutumia Kikamilifu App ya YouTube

Fahamu haya hapa maujanja mbalimbali ya app ya YouTube

Maujanja ya Jinsi ya Kutumia Kikamilifu App ya YouTube

Moja kati ya tovuti inayotumiwa na watu wengi zaidi duniani ni pamoja na tovuti ya YouTube, pamoja na watu wengi kutumia tovuti hiyo, pia App ya mtandao huo ni moja kati ya App inayo ongoza kwa kupakuliwa na watu wengi zaidi kwenye masoko ya Play Store na App Store.

Japokuwa App za mtandao huo ni maarufu sana ni watu wachache sana wanaojua njia mbalimbali au kama tunavyopenda kusema Maujanja ya kutumia App hizo kikamilifu. Leo Tanzania Tech tunakuletea maujanja mbalimbali ambayo yanaweza kufanya ufurahie zaidi kutumia App ya YouTube pia kama wewe unayo channel kupitia mtandao hup pia utaweza kufurahia maujanja haya pia. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie maujanja hayo..

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

1. Jinsi ya Kufanya App YouTube Isitumie MB nyingi

Ni kweli kwamba, kuangalia video kupitia Internet kunafanya utumie data kwa kasi kidogo, ndio maana kupitia app ya YouTube unaweza kufanya App hiyo isitumie data kwa kasi, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hizi.

Ingia kwenye App ya YouTube, kisha fungua sehemu ya Settings inayopatikana kwenye picha yako ya Profile Juu upande wa kulia. Bofya sehemu ya General, kisha angalia chini kidogo utaona maneno yaliyo andikwa Limit Mobile data usage, bofya hapo kuweza kuwasha sehemu hiyo. Sasa sehemu hii inafanya kazi ya kupunguza muonekano wa video ili kusaidi kutunza MB zako pale unapo angalia Video kupitia App ya YouTube.

2. Jinsi ya Kuangalia Video Zinazo Trendy Nchi Nyingine

Kama wewe ni mmoja ya watu wenye channel kwenye mtandao wa YouTube basi hii itakuwa ni nzuri sana kwako. Kama kwa namna yoyote video yako imekuwa Trendy hapa Tanzania na unataka kuangalia kama video hiyo ina trendy kwenye nchi kama kenya uganda na sehemu zingine duniani unaweza kufuata hatua hizi.

Fuata hatua za kuingia kwenye sehemu ya Settings kama ilivyo kwenye hatua hapo juu, kisha ingia General kama ilivyo hapo juu alafu shuka mpaka Sehemu iliyo andikwa Location, badilisha na weka nchi ambayo ungependa kuangalia kama video yako ina trendy, usisahau kubofya Menu ya Trending inayopatikana chini kidogo ya App hiyo ya YouTube.

3. Angalia Video kwa Nyuzi 360

Video za nyuzi 360 zimekuwa ni video ambazo zinapata umaarufu pole pole sana, pengine hii ni kutokana na watu wengi kutokujua kuhusu video hizi. Sasa kuna njia ambazo unaweza kuzipata video hizo na kupitia hatua hizi ndivyo utakavyoweza kuziona. Kwenye sehemu ya kutafuta andika jina la video unayotaka kutafuta, kisha bofya kitufe cha kutafuta, baada ya hapo bofya kitufe cha Filter kilichopo upande wa kulia, kisha chagua 360 kisha malizia kwa kubofya Apply.

Baada ya hapo hakikisha unaweka simu yako kwenye mfumo wa Horizontal, kisha  tembeza kidole chako kwenye video hiyo utaona inaonekana pande zote yani nyuma, mbele pamoja na pembeni ya video hiyo. Angalia video hapo chini…

Na hayo ndio maujanja ambayo nimekuandalia kwa siku ya leo, kama unajua maujanja mengine kwaajili ya App ya YouTube unaweza kutuambia kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu tutakuwa tunaongeza maujanja mengi zaidi pindi tutakapo yapata.

Fanya Hatua Hizi Kabla Simu Yako Haijapasuka Kioo

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment