Sehemu ya Facebook Watch Yaja Rasmi kwa Watumiaji Wote

Sasa unaweza kuangalia video mbalimbali kupitia sehemu ya Facebook Watch
Sehemu ya Facebook watch Sehemu ya Facebook watch

Hatimaye sehemu mpya ya Facebook Watch imetangazwa kuja rasmi kwa watumiaji wote, sehemu hiyo ambayo ilikuwa kwenye majaribio kwa nchini marekani, itakuruhusu kuangalia video mbalimbali zikiwa kwenye mfumo wa vipindi (Episode). Sehemu hii ilitangazwa ujio wake hapo mwaka jana na sasa iko tayari kwaajili ya watumiaji wote.

Facebook Watch inahusisha video za aina zote iwe ni video za habari, michezo au video za aina yoyote utaweza kuzipata kupitia Facebook Watch. Sehemu hiyo kwa sasa tayari iko kwenye app za Facebook, na hapa Tanzania Tech tayari tumesha weza kuona sehemu hiyo mapema wiki iliyopita.

Advertisement

Hata hivyo Facebook imetangaza kuwa sehemu hiyo itakuwa inapatikana kama TAB maalum ambayo itakuwa juu kabisa pale utakapo ingia kwenye app yako ya Facebook, pia unaweza kuipata kupitia sehemu ya mistari mitatu iliyoko upande wa kulia kisha angalia sehemu iliyoandikwa Watch, hii unaweza kuipata kupitia App ya mfumo wa Android.

Kama bado hujapata sehemu hii hakikisha una update app yako ya Facebook kupitia masoko yote ya Play Store na App Store.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use