in

WhatsApp Yawezesha Group Call Hadi Watu 4 kwa Pamoja

Sasa utaweza kupigia hadi watu wanne simu za sauti na video

WhatsApp Video Call

Mwezi wa tano mwaka huu 2018, Facebook kupitia mkutano wake wa F8 ilitangaza ujio sehemu ya Group Call, sehemu hiyo tayari imesha fika kwenye programu za WhatsApp na hivi leo WhatsApp kupitia blog yake imetangaza kuwa sasa utaweza kuwapigia simu za video hadi marafiki zako wanne kwa pamoja.

Mbali na hayo vilevile mtumiaji wa programu hiyo ya WhatsApp ataweza pia kuwapigia simu za sauti hadi watu wa nne kwa pamoja ndani ya programu ya WhatsApp. Sasa ili kuweza kuongeza mtu kwenye simu za video au za sauti, unatakiwa kumpigia mtu simu ya video au ya sauti, kisha kwenye kona juu upande wa kulia utaona kitufe cha kuweza kuongeza mtu na pale utakapo bofya hapo utaweza kuongeza mtu kwenye simu hiyo iwe ni video call au audio call.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa sasa tayari sehemu hii ipo kwenye programu za WhatsApp hivyo kama bado hujafanikiwa kuona sehemu hiyo basi hakikisha una sasisha (update) toleo jipya la programu hizo kupitia masoko ya Play Store au App Store.

Amani Joseph

WhatsApp Yawezesha Group Call Hadi Watu 4 kwa Pamoja

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment