Baadhi ya Simu za Huawei Zazuiwa Kudownload App ya VLC

Simu hizo hazitaweza kupakua app hiyo kupiti soko la Play Store
VLC kwenye Huawei VLC kwenye Huawei

VLC ni moja kati ya programu inayotumiwa na watu wengi sana kwenye vifaa mbambali, kama unavyojua VLC pia inazo app ambazo zinatumiwa na watu zaidi ya milioni moja kwenye mifumo mbalimbali ya Android pamoja na iOS.

Sasa hivi karibuni idadi ya watumiaji hao itaenda kupungua kutokana na sheria mpya ya kampuni ya VideoLAN, ambayo inaelekeza kuzuia simu za Huawei kupakua app ya VLC ya mfumo wa Android kupitia soko la Play Store. Hatua hii inakuja baada ya tweet kutoka kwenye akaunti ya kampuni hiyo ikielekeza sababu za kufanya hivyo ni kutokana na watumiaji wa App hiyo kutoa malalamiko ya programu hiyo kutofanyakazi vizuri.

Kwa mujibu wa Tweet hiyo, sababu hiyo ya kutokufanya kazi vizuri kwenye simu hizo za Huawei inasababishwa na aina mpya ya mfumo wa Huawei ambao unazuia app zilizoko kwenye simu hizo ikiwa pamoja na VLC kutofanyakazi kwa nyuma (Background) na hiyo kusababisha App hiyo kutofanya kazi vizuri.

Apps nyingi za mfumo wa android huwa na tabia ya kuendelea kufanya kazi kwa nyuma hata kama huitumii na hii inafanya app hizo kufanya kazi vizuri pale unapoifungua kwa mara ya pili, lakini pia hii inasababisha simu nyingi kuisha chaji kwa haraka, ndio maana kampuni ya Huawei imekuja na mfumo huo ambao unazima Apps zote ambazo zinafanya kazi kwa nyuma hata kama hazitumiki.

Hata hivyo kampuni ya VideoLAN haijatoa list ya simu ambazo hazitaweza kupakua app hiyo, lakini kwa mujibu wa muendelezo wa tweet hiyo simu nyingi mpya za Huawei ndizo zitakazo adhiriwa na mabadiliko haya ikiwa pamoja na Simu za Huawei P8, Huawei P10 na Huawei P20.

Kwa sasa kama wewe ni mtumiaji wa simu hizo za Huawei unaweza kupakua app hiyo kupitia tovuti nyingine zenye kuruhusu kupakua file za APK za mfumo wa Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use