in

Facebook na Cristiano Ronaldo Kuleta Kipindi Kipya cha TV

Kipindi kipya chenye kuonyesha maisha ya Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo

Facebook sasa imeamua kuangalia upande mwingine na kuamua kufanya uwekezaji kwa mchezaji maarufu kutoka klabu ya mpira wa miguu ya Real Madrid mwenye asili ya kireno, Cristiano Ronaldo. Kwa mujibu wa habari kutoka tovuti ya Variety, Facebook inatarajia kuanzisha kipindi kipya kabisa kitakachokuwa kinaonyesha maisha halisi ya mchezaji huyo ndani na nje ya uwanja wa mpira.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Cristiano Ronaldo anategemewa kulipwa na Facebook kiasi cha dollar za marekani zaidi ya milioni 10 sawa na Tsh Bilioni 22.5 kwaajii ya kipindi hicho cha TV ambacho kitakuwa na sehemu 13. Hata hivyo bado tetesi zinasema kuwa mazungumzo kati ya mchezaji huyo na kampuni ya Facebook yanaendelea hivyo inawezekana mchezaji huyo akalipwa dau kubwa zaidi ya hilo lililotajwa.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa Forbes, kwa sasa Cristiano Ronaldo anautajiri wa zaidi ya dollar za kimarekani milioni 108 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania bilioni 245.6 huku akiwa ni kati ya wachezaji wa mpira wa miguu wanaolipwa vizuri zaidi duniani.

Hata hivyo kwa mujibu wa Variety, kipindi hicho chenye kuonyesha maisha ya mchezaji huyo kitakuwa kinaonyeshwa kupitia mtandao wa Facebook kwenye sehemu ya Facebook Watch sehemu iliyozinduliwa mwaka jana kwaajili ya kuangalia Video, Tamthilia, Habari pamoja na vipindi mbalimbali. Kwa sasa Facebook Watch haipo kwa Tanzania ila unaweza kuitazama kwa kutumia programu maalum za VPN.

Tigo 5G Sasa Inapatikana Dar es salaam, Dodoma na Zanzibar

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.