in

Tetesi : Muonekana wa Simu Mpya ya iPhone SE 2 (2018)

Simu hii inatarajiwa kuja na ukingo wa juu

Tetesi : Muonekana wa Simu Mpya ya iPhone SE 2 (2018)

iPhone SE ni simu kutoka kampuni ya Apple ambayo ilizinduliwa mwaka 2016, tokea kipindi hicho hadi sasa kampuni ya Apple haikuwai kutoa toleo jipya la simu hiyo ambayo iliuza nakala nyingi zaidi mwaka 2016 na kufanya mauzo ya simu kutoka Apple kuongezeka kwa asilimia 5.1.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi za ujio mpya wa simu hiyo ya iPhone SE 2 (2018) na toka tetesi hizo zimeanza hadi sasa leo ndio tumeona ni wakati sasa wa kukujuza kuhusu simu hiyo baada ya kupata ushahidi kweli simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni. Kupitia ukurasa wa Twitter wa kampuni maarufu ya kuuza vifaa vya simu za mkononi ya Mobile Fun, kumekuwa na picha ambayo inasemekana ndio muonekano halisi wa simu hiyo ya iPhone SE 2 (2018) inayo semekana kuzinduliwa mwezi unaokuja.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa tetesi hizo kama unavyo ona kwenye picha hapo juu iPhone SE 2 (2018)  inategemewa kuja na ukingo wa juu maarufu kama Notch kama ilivyo simu ya iPhone X, pia simu hii itakuja na kioo kisicho na ukingo, lakini kwa upande wa muundo iPhone SE 2 (2018) inatarajiwa kuja na muundo unao lingana sana na ule muonekano wa iPhone SE ya mwaka 2016.

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili kuhusu tarehe halisi ya kutoka kwa simu hii, lakini wataalamu wa maswala ya teknolojia wanasema kuwa simu hii inatarajiwa kuzinduliwa kwenye mkutano wa Apple maarufu kama WWDC 2018, ambao unafanyika kila mwaka mwezi wa sita ambapo hapo kampuni ya Apple hupata nafasi ya kutambulisha bidhaa mbalimbali kwa wapenzi na watumiaji wa bidhaa mbalimbali za Apple.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments