in

Hatimaye Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia 6.1 Plus (2018)

Zifahamu sifa pamoja na bei za simu hii mpya kutoka Nokia

Sifa na Bei ya Nokia X6 (2018)

Baada ya Tetesi za muda mrefu kuhusu Simu mpya ya Nokia X6 (2018), Hivi leo kampuni ya Nokia kupitia HMD Global imetangaza kuzindua rasmi simu hiyo huko nchini China. Kama tetesi zilivyokuwa zinasema simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma bila kusahau ukingo wa juu maarufu kama notch.

Simu hii pia inakuja na kioo cha touchscreen chenye ukubwa wa inch 5.8 pamoja na aspect ratio ya 19:9. Vilevile simu hii ya Nokia X6 (2018) inakuja na processor ya Snapdragon 636 SoC chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6 pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8.1 Oreo.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Nokia X6 (2018)

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya IPS LCD display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~435 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260, Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipest.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 509
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 32 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na RAM ya GB 4 na nyingine itakuwa na RAM ya GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye ((f/2.0, 1.0µm).
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ina Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/2.0, 1.0µm, giro-EIS) na nyingine yenye Megapixel 5 yenye (f/2.2, 1.2µm), kamera zote zina uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3060 mAh battery yenye uwezo wa Fast battery charging (Quick Charge 3.0).
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue pamoja na White.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za DHybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Utaweza kununua Nokia X6 (2018) kuanzia tarehe 21 May nchini China na bei yake itaanzia Yuan ya china CNY1,299 ($204) sawa na Shilingi za kitanzania Tsh 466,000 kwa Nokia X6 ya RAM ya 4GB na Ukubwa wa ndani wa GB 32. Toleo la Nokia X6 lenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani ya GB 64 yenyewe itauzwa kwa Yuan ya china CNY1,449 ($236), sawa na Tsh 539,000.

Toleo lingine la mwisho la Nokia X6 lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 64 utaweza kuinunua kwa Yuan ya china CNY1,699 ($266) sawa na shilingi za Tanzania Tsh 608,000. Kuhusu upatikanaji bado HMD Global haija tangaza kuhusu ujio wa simu hii kwa nchi nyingine zaidi ya China. endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi tutakapo pata taarifa za simu hii kuja Afrika na ikiwa pamoja na Afrika mashariki kwa ujumla.

Angalia Uzinduzi wa iPhone 15 Ndani ya Dakika 17

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.