in

Samsung Kuja na Galaxy S9 na S9 Plus za GB 128 na GB 256

Simu hizo kwa sasa zitakuwa zinapatikana kwa nchini Marekani Pekee

Galaxy S9 na S9 Plus

Kampuni ya Samsung imetangaza rasmi kuwa, inatarajia kuzindua simu mpya za Samsung Galaxy S9 pamoja na Galaxy S9 Plus ambazo zitakuwa na ukubwa wa ndani wa GB 128 pamoja na GB 256. Hapo awali simu hizo zilikuwa na machaguo mawili ya ukubwa wa ndani wa GB 64 pamoja na GB 32 Pekee.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, Simu hizo mpya zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kupitia tovuti ya Samsung siku ya ijumaa ya mwezi May tarehe 18 na kwa sasa tayari utakuwa na uwezo wa kuagiza simu hizo moja kwa moja kupitia tovuti ya samsung.com.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo bado hakuna ripoti kama simu hizo zita patikana nchi nyingine nje ya Marekani, kwani siku ya jana Samsung ilitangaza kuwa, kwa sasa simu hizo zitapatikana kwa nchini Marekani pekee na zitapatika kwa bei ya dollar za Marekani $769.99 sawa na Tsh 1,733,000, kwa Galaxy S9 yenye GB 128 na dollar $819.99 sawa na Tsh 1,845,000 kwa Galaxy S9 yenye GB 256.

Kwa upande wa Galaxy S9 Plus yenyewe itakuja ikiwa inauzwa dollar $889.99 sawa na Tsh 2,033,000 kwa Galaxy S9 Plus yenye GB 128 na dollar $939.99 sawa na Tsh 2,147,000 kwa Galaxy S9 Plus yenye GB 256. Simu zote zinategemewa kuja na sifa zilezile za kawaida na zina tegemewa kuwa na machaguo matatu ya rangi za Lilac Purple, Coral Blue, pamoja na Midnight Black.

Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi Samsung watakapo tangaza kuhusu ujio wa simu hizo kwenye nchi nyingine zikiwemo nchi za Afrika Mashariki.

Amani Joseph

Samsung Kuja na Galaxy S9 na S9 Plus za GB 128 na GB 256

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apple Yathibitisha iPhone 15 Kuzinduliwa 12 Septemba

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.