in

Sasa Unaweza Kujaribu App ya Kuchati ya Instagram Direct

Sasa unaweza kuchati kupita App Tofauti na sehemu ya DM

App ya Instagram Direct
Muonekano wa App ya Direct Kutoka Instagram

Miezi kadhaa iliyopita tulitoa taarifa za mtandao wa Instagram kuja na App maalum kwaajili ya kuchat inayo itwa Direct. Baada ya kuijaribu na kutumia App hii kwa muda mrefu leo nimeona nikujuze angalau kidogo kuhusu app hiyo mpya kutoka Instagram.

Kwa muundo jinsi App hiyo ilivyo ni kama App ya Instagram, unaweza kuchati kama ilivyo kwenye app ya Instagram na pia unaweza kufanya kila kitu kama ilivyo kwenye sehemu ya DM kupitia App ya Instagram. Binafsi yangu sijaona tofauti kati ya App hii ya Direct pamoja na sehemu ya DM kwenye app ya Instagram. Labda wewe unaweza kuniambia baada ya kujaribu App hii.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sasa ili kujaribu App hii kama unatumia simu ya mfumo wa Android unatakiwa kupakua app hiyo kwa kutumia link hiyo hapo chini, link hiyo siyo ya Play Store na sababu za kuweka link ya aina hiyo ni kuwa, kwa sasa App hiyo inajaribiwa kwa nchi chache na Tanzania au nchi za Afrika mashariki sio moja ya nchi hizo, Hivyo ni lazima kupakua file la apk ili kuweza kujaribu App hiyo.

Direct From Instagram

Kwa watumiaji wa iOS inakubidi kuingia kwenye soko la App Store kisha bofya picha yako Juu upande wa kulia kisha bofya kwenye akaunti yako yenye jina lako na barua pepe yako, kisha bofya Country/Region kisha hapo badilisha nchi kwenda kwenye nchi ya Uruguay. Sababu za kufanya hivi ni kama nilivyo sema hapo juu, App hiyo inajaribiwa kwa nchi chache na Tanzania sio moja ya nchi hizo. Baada ya kufuata hatua zote hizo ingia kwenye tovuti ya Tanzania Tech kwa kutumia kivinjari cha Safari fungua makala hii kisha bofya link hapo chini.

Direct From Instagram

Kama kuna mahali umekwama tuambie kwenye maoni hapo chini tutakusaidia, lakini kama umeweza kupakua App hii tuambie maoni yako unaonaje App hiyo..?

Amani Joseph

Sasa Unaweza Kujaribu App ya Kuchati ya Instagram Direct

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

OpenAI Mbioni Kuingiza Takribani Dola Bilioni 1 Kwa Miezi 12

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments