in

Ripoti : Instagram Kuanza Majaribio ya App Mpya Kwaajili ya Kuchat

Sasa utaweza kuchat na kutumia Camera nje ya App ya Instagram

App ya Direct
Picha za App Mpya ya Instagram ya Direct.

Hivi karibuni ripoti zimetoka kuptia tovuti mbalimbali zikisema kuwa mtandao wa Instagram sasa unafanyia majaribio App mpya kwaajili ya simu ambayo itakuwa ni kwaajili ya kuchat.

Ripoti hizo kutoka tovuti ya The Verge zinasema kuwa, App hiyo ambayo inaitwa “Direct” itakuwa inatenganisha sehemu ya kuchat iliyopo kwenye programu ya kawaida ya Instagram na kama ilivyo kwenye programu za simu za facebook Messenger, ili kuchati itakubidi kuwa na App hiyo ya direct ambapo utaweza kuchat na marafiki walio kufuata au ulio wafuata kupitia akaunti yako ya instagram.

Programu hiyo yenye sehemu ya Camera kama ilivyo snapchat inategemewa kuanza kujaribiwa kuanzia siku ya leo kupitia mifumo yote ya Android na iOS kwa nchi za Chile, Israel, Italy, Portugal, Turkey pamoja na Uruguay.

Ingawa Instagram imeanza majaribio ya App hiyo mpya ni mapema sana kusema ni lini programu hiyo itakuja kwa watumiaji wote, lakini pengine programu hii ikifanikiwa kwenye majaribio yake kupitia nchi hizo sita, basi watumiaji wa programu ya Instagram wajiandae kutumia App ya Instagram bila sehemu ya DM.

Vipi unaonaje Instagram kufikia hatua hii ya kutenganisha sehemu ya DM na App ya Instagram..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.