in

Jiandae na Simu ya Kwanza Yenye Android Go Kutoka Samsung

Simu hiyo itakuja na uwezo wa RAM ya GB 1

Jiandae na Simu ya Kwanza Yenye Android Go Kutoka Samsung

Android Go ni mfumo maalumu wa Android kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo, Mara nyingi simu zenye mfumo huu huwa na uwezo wa RAM kuanzia GB 1 kushuka chini. Hata hivyo mfumo huu umetengenezwa maalum kwaajili ya kuwezesha watu wengi zaidi kutumia mfumo wa Android, hata wale wanao pendelea simu za bei rahisi.

Sasa tumesha sikia baadhi ya kampuni za simu zikizindua simu zao zenye mfumo wa Android Go, lakini kwa Samsung bado tunaendelea kusubiri simu hiyo. Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, huenda utaipata simu ya kwanza yenye mfumo huo sababu simu yenye uwezo mdogo unaolingana na simu zenye mfumo huo wa Android Go, imeonekana kwenye tovuti ya Geekbench. Geekbench ni kampuni maalum kwaajili ya kupima vifaa mbalimbali vya kieletroniki ili kujua uwezo wa vifaa hivyo ili kutathimini kama vifaa hivyo viko tayari kuingia sokoni.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu yenye modeli namba ya Samsung SM-J260G iko kwenye majaribio kupitia Geekbench na inasemekana simu hiyo itakuja na mfumo huo kutokana na kuandikwa kwenye tovuti hiyo ya Geekbench ikiwa na uwezo wa RAM ya GB 1. Sasa wote tunajua kuwa samsung haiwezi kuja na simu mpya yenye RAM ya GB 1, isipokua kama simu hiyo itakuwa inatumia mfumo wa Android Go.

Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, simu hiyo inaonekana kuwa na RAM ya MB 846 sawa na GB 1, lakini inatumia mfumo wa Android 8.1.0 hivyo ni wazi kuwa simu hii itakuwa inatumia mfumo wa Android Go (Oreo 8.1). Ingawa simu hiyo inasemekana kuja na mfumo wa Android Go ambao ni mfumo maalumu kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo, lakini inasemekana kuwa simu hii itakuja na uwezo mkubwa wa Processor kama ilivyo simu ya Samsung Galaxy J2.

Kwa sasa hakuna ripoti kamaili kuhusu simu hiyo itakuwa ni simu gani, lakini ni uhakika kuwa Samsung inajiandaa kuja na simu yenye uwezo wa Android Go, hivyo tegemea kuipata simu hiyo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Yote ya Muhumu Kuhusu iPhone 15 kutoka Apple

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.