in

Zifahamu Hizi Hapa Bei na Sifa za Tecno Camon X (2018)

Ni bora lakini Pengine kamera za simu hii sio kama wengi walivyodhani

Sifa za Tecno Camon X

Kampuni ya Tecno Tayari imesha zindua simu mpya za Tecno Camon X (2018) pamoja na Tecno Camon X Pro, Tanzania Tech tumesha fanikiwa kupata muonekano wa simu hiyo pamoja na sifa kamili za simu hiyo. Kwenye makala hii utaenda kuzifahamu sifa za simu hiyo inayotegemewa kuzinduliwa leo huko nchini Nigeria.

Kama unavyo ona kwenye picha simu hii ya Tecno Camon X inakuja na kioo cha kisasa cha full display chenye aspect ratio ya 18:9 pamoja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android 8.1 Oreo pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Tecno Camon X

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 1080 x 2160 pixels, 18:9 ratio (~269 ppi density)
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0GHz MediaTek Helio P23
 • Uwezo wa GPU – Mali-T720
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16 kwa Tecno Camon X na GB 64 kwa Tecno Camon X Pro zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
 • Ukubwa wa RAM – GB 3 kwa Tecno Camon X na GB 4 kwa Tecno Camon X Pro
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 kwa Tecno Camon X Pro na Megapixel 20 kwa Tecno Camon X zote zikiwa na Ring flash
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 ikiwa na Dual-flash
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3750 mAh battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
  pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0
 • Rangi – Inakuja kwa rangi ya Midnight Black
 • Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
 • Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G

Kuhusu Bei, Simu hizi zitauzwa kwa Tsh 550,000 hadi Tsh 470,000 kwa Tecno Camon X, na Tsh 700,000 hadi Tsh 600,000 kwa Tecno Camon X Pro. Kwa sasa unaweza kupata simu hii kupitia soko la matandao la Jumia.

Kwa habari zaidi za simu hii ikiwa pamoja na mahali pa kuipata pamoja na bei zake endelea kutembelea Tanzania Tech.

Angalia Uzinduzi wa iPhone 15 Ndani ya Dakika 17

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

14 Comments