in

Programu 5 Bora za Visakuzi Kwenye Simu na Kompyuta 2019

Fungua kurasa za mitandao mbalimbali kwa haraka kwa kutumia visakuzi hivi

Visakuzi Browser Bora 2018

Ni wazi kuwa wote tunatumia visakuzi au (Browser) kuperuzi kwenye mtandao, kutokana na visakuzi kuwa sehemu muhimu ya matumizi yetu ya mtandaoni basi leo nimekuletea programu bora za visakuzi ambazo unaweza kutumia kwenye simu au kompyuta yako ili kuperuzi mtandao kwa haraka.

5. Puffin Browser

Puffin browser ni moja kati ya visakuzi bora sana kwa sasa, kisakuzi hichi ni kizuri kwa mfumo wake pia kinauwezo wa kufungua kurasa za mitandao unayo peruzi kwa haraka zaidi. Kisakuzi hichi sasa kimeanza kupatikana kwa watumiaji wa mfumo wa Windows na tayari pia kinapatikana kwenye soko la Play Store kwaajili ya watumiaji wa simu za Android.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Download Puffin Browser

4. Brave Browser: Fast AdBlocker

Kisakuzi cha Brave Browser ni moja kati ya visakuzi bora kwa sasa na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuzuia matangazo yanayo kera kwenye tovuti mbalimbali. Kisakuzi hichi pia kinauwezo wa kuzuia mitandao mbalimbali ikiwa pamoja na kuzuia watu kuchunguza matumizi yako ya internet au mtandao fulani. Kizuri kuhusu kisakuzi hichi kipataikana kwenye mifumo yote ya kompyuta, Android pamoja na iOS.

Download Brave Browser

3. Google Chrome

Kisakuzi cha kingine kwenye list hii ni Google chrome pangine kwa sasa hichi ndio kisakuzi kinacho tumiwa na watu wengi sababu ya kuwa kisakuzi cha muhimu kwenye simu za Android. Lakini tofauti na visakuzi vingine kisakuzi hichi hakina huwezo wakutosha kwenye kompyuta zenye uwezo mdogo ikiwa pamoja na simu zenye uwezo mdogo wa RAM. Mbali na hayo machache kisakuzi hichi ni bora na sasa kime ongezewa sehemu nyingine mpya ya kuzuia matangazo unaweza kusoma hapa kujua zaidi.

Download Chrome Browser 

2. Opera Browser

Kisakuzi kingine ambacho ni bora kwa sasa ni kiasakuzi cha Opera, kiasakuzi hichi ambacho kimedumu kwa muda mrefu ni moja kati ya visakuzi vyenye umri mkubwa zaidi lakini pia ni moja kati ya visakuzi vyenye uwezo wa kuzia matangazo pamoja na kuzuia mtu kuangalia matumizi yako ya mtandao ikiwa pamoja na kufungua kurasa za mtandao kwa haraka zaidi.

Download Opera Browser

1. Firefox Browser

FireFox ni moja kati ya visakuzi bora sana kwa sasa kisakuzi hichi kipya kinauwezo wa kufanya kazi kwenye vifaa vyenye uwezo mdogo ikiwa ni kompyuta pamoja na simu za mkononi maarufu kama Smartphone. Kisakuzi hichi kipya sasa kinasifika na kinauwezo mkubwa sana wa kufungua kurasa za mitandao unayo itembelea kwa haraka na kwa kasi ya hali ya juu. Jaribu sasa kisakuzi hichi kipya cha Firefox

Download Firefox Browser

Na hizo ndio programu bora za visakuzi ambazo nahisi unaweza kufurahia kutumia, Tuambie ni kisakuzi gani unatumia na ni kwasababu gani.? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Apps Nzuri Kwaajili ya Kupakua Video za Aina Yoyote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.