Aina Mpya ya Virusi Vinavyo Athiri Kompyuta za Mfumo wa macOS

Mpaka sasa bado hakuna njia wala programu yoyote ya kuzuia na virusi hivi
Kompyuta ya Macos Kompyuta ya Macos

Siku za karibuni kumegundulika aina mpya mbalimbali za virusi lakini aina hii mpya ya virusi ni mpya kabisa kwenye mfumo wa macOS, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa The Hacker News, aina mpya ya virusi vimegundulika ambavyo vina uwezo wa kuchukua screenshot kwenye kompyuta yako kufungua ma-file mbambali pamoja na mengine mengi.

Virusi hivyo vina uwezo wa kubadilisha mfumo wa DNS Server kwenye kompyuta iliyoadhiriwa mfumo ambao ndio hutumika wakati unatumia internet, baada ya kubadilisha mfumo huo hupitisha matumizi yako ya internet kwenye Server zilizo adhiriwa na virus na wakati kitendo hichi kinatokea virusi hivyo vinaweza kuchukua data za muhimu kutoka kwenye kompyuta yako ya Mac.

Aina hii ya virusi kwa sasa imepewa jina la OSX/MaMi. Hata hivyo baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kufanywa na virusi hivi vikiadhiri kompyuta yako ni pamoja na kuchukua picha za matumizi ya kompyuta yako, ku-upload na kudownload file la aina yoyote kutoka kwenye kompyuta yako pamoja na kuwasha au kufuta programu yoyote kwenye kompyuta yako.

Advertisement

Ili kujua kama kompyuta yako imeadhiriwa ama lah!. Sasa ili kujua, ingia kwenye sehemu ya System Preferences kwenye kompyuta yako ya Mac kisha nenda kwenye Network Menu alafu bofya “Advanced” alafu bofya sehemu ya DNS kisha angalia namba hizi 82.163.143.135 na 82.163.142.137 kama zipo basi kompyuta yako imeadhiriwa.

Mpaka sasa bado hakuna programu yoyote ya Anti-virus yenye uwezo wa kugundua virusi hivi na pia bado hakuna taarifa yoyote juu ya virusi hivi vilipo anzia ikiwa ni pamoja na njia za kuzuia kompyuta yako isiadhiriwe na virusi hivi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use