in

BlackBerry Kuja na Simu Mpya Nyingine ya BlackBerry Motion

Hii ndio simu mpya ya Touch kutoka kampuni ya Blackberry

Blackberry Motion

Blackberry ni moja kati ya kampuni ambayo ili kuwa maarufu sana miaka ya 90 wakati simu zake janja ndio silikuwa simu bora kuliko simu nyingine. Lakini kufikia mwaka 2004 android ili zaliwa na kufanya kampuni hiyo kushuka na kuwa moja kati ya kampuni za simu zinazofanya vibaya.

Lakini kufikia mwaka huu 2017 Blackberry imendela kujiunga na Android na kutoa simu zake tofauti ikiwepo simu iliyotoka mwaka jana ya Blackberry Key One, pamoja na uzinduzi wa simu hiyo bado simu hiyo haikufanya vizuri sana na hatimaye kampuni hiyo sasa imerudi na simu mpya ya Blackberry Motion.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hiyo mpya ambayo sasa bado haijaingia rasmi sokoni, inasemekana kuwa imetengenezwa kwa muungano wa kampuni za TCL pamoja na kampuni ya Blackberry na inasemekana kuja na sifa za kisasa na maboresho zaidi ikiwa pamoja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi au water and dust resistant.

Mbali na hayo simu hiyo ya Blackberry Motion inasemakana kuja na kioo cha inch 5.5 full HD pamoja na RAM ya GB 4 huku ikiendeshwa na Battery kubwa ya 4000mAh yenye teknolojia ya QuickCharge 3.0 huku ikiwa na uwezo wa kukaa na chaji masaa 32 kwa mujibu wa kampuni hiyo.

Simu hiyo ambayo imezinduliwa leo inasemekana kuja na uwezo wa kutumia line mbili za simu huku ikiwa ndio simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo ikiwa na uwezo huo. Kujua sifa kamili za Blackberry Motion bofya hapa.

Kwa upande wa Bei Blackberry Motion itauzwa kwa dollar za marekani $460 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,032,148 kwa mujibu wa viwango vya fedha vya leo kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : TechRadar

Google Kuzindua Simu Mpya za Pixel 8 Mwezi Oktoba (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.