in

Programu 5 Zinazoweza Kusaidia Kupunguza Simu Kupata Moto

Simu yako inapata moto mara kwa mara basi tumia programu hizi

Simu kupata Moto

Simu kupata moto inaweza kuwa ni dalili ya simu yako kupata shida fulani lakini pia kuna wakati kupata huko moto kuna sababishwa na mambo ambayo unaweza kuyazuia na kurudisha simu yako kwenye hali ya kawaida.

Kusaidia kwenye hilo leo ninakuletea programu hizi tano ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia pale simu yako inapo pata moto kupita kiasi, kama ambavyo tulisema hapa tanzania tech yapo matatizo mbalimbali yanao sababishwa na simu kupata moto unaweza kusoma matatizo hayo hapa kama ulipitwa na hii.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Moja kwa moja twende tukangalie programu hizi tano ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kusaidia kutuliza au kupunguza joto kwenye simu yako ya Android.

5. Coolify

Coolify
Price: Free

Coolify ni programu ambayo kaziyake kubwa nikuhakikisha simu yako inakuwa kwenye joto la kawaida, pindi programu hii itakapo gundua kuwa simu yako ina joto kali zaidi ya kawaida basi itakuleta taarifa ili uweze kuiruhusu programu hiyo kupunguza joto la simu yako.

4. Device Cooler – Cooling Master

Programu hii pia ni programu ambayo huangalia hali ya joto la simu yako kisha kukupa taarifa ya kuruhusu programu hii kupunguza joto la simu yako, lakini tofauti na programu ya Coolify hii inafanya kazi ya kufunga programu ambazo zinatumia kiasi kikubwa cha RAM ambapo pengine ndio chanzo cha simu yako kupata joto.

3. Device Cooler Heat Minimizer

Hii ni programu nyingine ambayo yenyewe hufanya kazi ya kupunguza joto kwenye simu yako kwa kuhakikisha inazima programu zote ambazo zinatumia kiasi kikubwa cha RAM pamoja na CPU, programu hii ni ya kisasa na imethibitika kufanya kazi kwenye simu nyingi zenye tatizo hili

2. Cooling Master-Phone Cooler

Hii ni moja kati ya programu ambazo zimeonekana kusaidia watu wengi sana wenye simu zinazopata joto pamoja na kutoa taarifa pale joto la kwenye simu yako litakapo kuwa sio la kawaida.

1. Clean Master- Space Cleaner & Antivirus & Free Ram

Programu hii ni moja kati ya programu za muhimu sana kwenye simu, umuhimu wake haishi kwenye kuzuia simu yako kupata joto bali pia kwenye kuongeza ufanisi mkubwa kwenye simu yako. Programu hii inasaidia kwa kuondoa baadhi ya mafaili ambayo yanajaa kwenye simu yako ambayo hunyima nafasi simu yako kuhifadhi faili zingine na kusababisha simu kupata joto sana, kifupi ni kuwa programu hii ni ya lazima sana kuwa nayo.

Pamoja na programu hizi ni vyema kufuata baadhi ya kanuni ili kuzuia simu yako kupata joto, baadhi ya njia hizo ni kama vile kuhakikisha simu inachajiwa na chaji yake, kutokutumia programu nyingi kwa wakati mmoja, kutoku kutumia simu yako kwa muda mrefu, kutokuweka kava ambalo linazuia simu yako kutoa kutoa joto nje na mengine mengi ambayo tutaya ongelea kwenye somo lijalo. Basi na hizo ndio programu ambazo ukitumia lazima utakuwa umesaidia simu yako kupunguza jashoooo linalotokana na joto kali.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Jinsi ya Kutengeneza Akaunti ya Threads Hatua kwa Hatua

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments