Video: Hii Hapa Ndio Simu Mpya ya iPhone 8 Inayotoka September

Baada ya tetesi za muda mrefu sasa huu ndio muonekano halisi wa iphone 8
iphone 8 iphone 8

Baada ya tetesi za hapa na pale pamoja na maongezi mengi sana kuhusu muonekano pamoja na sifa za iphone 8, sasa leo tunakuletea hii ambapo inadhibitishwa huu ndio muonekano wa simu mpya ya iphone 8 ambayo inategemewa kutoka mwezi september mwaka huu.

Wakati shukurani zikiwaendea mabingwa wa kuvujisha habari kuhusu bidhaa za apple Steve Hemmerstoffer na group lake, muonekano huu unatupa nafasi ya kuona simu hiyo kwa ukaribu pamoja na kuweza kuhakiki baadhi ya sifa ambazo awali zilikua ni tetesi tu kutoka kwenye mitandao mbalimbali.

Advertisement

Kupitia video hiyo tumeona apple wameongeza kioo cha simu hiyo ikiwa ni pamoja na kuficha kibonyezo cha katika kwenye kioo ambapo inasemekana pia fingerprint sasa itakuwa kwenye kioo pia mahali ambapo kibonyezo cha katika maarufu kama (Home Botton) kilipo kwepo. Kwa upande wa ukubwa wa simu hiyo kwenye video hiyo tumeona simu hiyo ikipimwa na kuonyesha ukubwa wa 71mm x 143mm x 7.4mm ambapo ni karibia kidogo na usawa wa iphone 7.

Kwa sasa bado tunahesabu mwezi na siku chache kwa siku hiyo kutangazwa rasmi ambapo tunategemea kuona muonekano huu au zaidi kwenye uzinduzi huo ambao tutakuletea matangazo yake moja kwa moja mubashara kupitia tovuti hii hivyo usicheze mbali kaa nasi…

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments
  1. Maoni*simu hizi za iPhone ziko vinzuri na katika ushidani WA soko utakuwa kiwango kinzurikupata ushidi. ubora wake uko vinzuri / naitwa JUMANNE salum kigalila

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use