Google Yakusaidia Kutunza Kiasi cha Data Kwenye Simu ya Android

Sasa unaweza kutunza kiasi cha data unazotumia kwa kutumia app mpya
triangle triangle

Wote tunajua kero inayotokana na kukatika kwa data ghafla tena pale unapokua huna hela ya kununua bando au uko mahali ambapo huwezi kupata bando, ndio maana google wamelifikiria hilo na kuleta app mpya ambayo itakusaidia kutunza kiasi cha data unazotumia kwenye simu yako ya mkononi ya Android.

App hiyo hiyo ya Triangle ambayo kwa sasa ipo kwenye majaribio inauwezo mkubwa sana wa kutunza data kwenye simu yako huku ikizuia app au programu ambazo zinatumia data bila wewe kujua. Kwasasa app hii ya Triangle inapatika kwa nchi za india pekee huku google wakiendelea kuiboresha na kufanya majaribio ya hapa na pale.

Lakini kwa sababu sisi na wengi wetu hapa tuko afrika basi tunakuletea app hiyo ambayo unaweza kuidownload sasa moja kwa moja kupitia ukurasa huu kwenye simu yako ya Android ili kuona jinsi app hiyo inavyo saidia. Mimi binafsi yangu nimeipenda sana programu hii kwani inatoa huduma ambayo sidhani kama kuna app nyingine inayofanya pamoja na kwamba kulikuwepo njia nyingine za kutunza kiasi cha data kwenye simu yako.

Advertisement

Kwa sasa unaweza kudownload app hii KUPITIA HAPA kisha install kwenye simu yako kisha fuata maelekezo ambayo yanakuelekeza kupitia kwenye app hiyo. Maelezo yake ni marahisi sana na inaweza kutumiwa na mtu yoyote mwenye simu ya Android.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use