in

Tetesi Note 8 Kuja na Kamera Mbili Zenye Nguvu Kuliko za iPhone

Baada ya kutoka kwa galaxy s8 sasa tetesi za galaxy note 8 ndio zimeanza

Galaxy Note 8

Baada ya kutoka kwa simu mpya ya Samsung Galaxy S8 sasa tetesi za simu mpya kutoka Samsung yaani Galaxy Note 8 ndio zimeanza, wiki hii mchambuzi maarufu wa usalama kutoka kampuni ya KGI anae julikana kwa jina la Ming-Chi Kuo, ameiambia tovuti ya 9to5google kuwa Galaxy Note 8 inategemea kuja na kamera mbili maarufu kama (Dual Camera) zenye nguvu zaidi ya zile za kwenye simu za iphone 7 plus.

Katika maongezi yake na tovuti hiyo Kuo amesema Samsung inategemea kuleta kamera hizo kwenye simu hiyo ya Note 8 uku zikiwa na uwezo wa 12-megapixel wide angle na nyingine 13-megapixel telephoto shots zenye uwezo wa 3x optical zoom. Ming-Chi Kuo anajulika sana kwenye mtandao kwa kutoa tetesi za kweli za simu za Apple na pia amejulikana sana kwa kutoa tetesi za simu za Samsung. unaweza kusoma tetesi zaidi kutoka kwake kupitia tovuti ya Macrumors.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Tetesi Note 8 Kuja na Kamera Mbili Zenye Nguvu Kuliko za iPhone

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apple Yathibitisha iPhone 15 Kuzinduliwa 12 Septemba

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.