in

Sasa Unaweza Ku-qoute Meseji Kwenye Whatsapp

whatsapp qoute

Programu bora ya kuchat ya Whatsapp sasa inauwezo wa ku-qoute meseji pale unapokua unachati, sehemu hii mpya ya programu hiyo inasaidia sana hasa kwa wale wanao chati kwenye ma-group mbalimbali kwa mfano inawezekana labda ujasoma meseji zako za whatsapp kwa muda mrefu na imetokea umekuta meseji zaidi ya 100 labda meseji moja au mbili zinakuitaji kujibu hapo inakuwa tatizo kidogo tena ikitegemewa kuwa tayari watu walisha endelea kuzungumzia mambo mengine kwenye group hilo.

Lakini kwa kutumia sehemu hii mpya unakua na uwezo wa kujibu meseji ya mtu hata kama ilikupita muda mrefu, ili kujua kama sehemu hiyo imewezeshwa kwenye simu yako ingia kwenye programu yako ya whatsapp kisha kwenye meseji unayotaka kujibu au ku-qoute kisha bofya na ushikilie kwa sekunde moja kisha utaona mshale wenye alama kama unaelekea upande wa kushoto bofya hapo na utaona meseji ya mtu unayetaka ku-qoute ikipanda juu na hapo itakupa uwezo wa kujibu meseji ya mtu huyo ikiwamo na meseji uliyoandikiwa hapo awali.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama bado huja pata sehemu hii muhimu unaweza ku-uninstall au kufuta programu  hiyo ya whatsapp na ku-install tena upya kisha kama bado hujaiona sehemu hiyo subiri kwa siku kadhaa kisha ujaribu tena.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog.

Sasa Unaweza Ku-qoute Meseji Kwenye Whatsapp
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Hizi Hapa Browser Bora Zenye Mfumo wa Akili Bandia (AI)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment