Yaliyojiri Kwenye Mkutano wa Google I/O Keynote

Google Google

Kama Jana haukuweza kuangalia sehemu ya kwanza ya mkutano wa kampuni ya google ambapo ulifanyika jana haya ndio yaliyojiri kwenye mkutano huo siku ya jana.

  • Uzinduzi wa Kifaa cha Google Home

2

Baada ya kampuni ya Amazon kutengeneza kifaa cha Amazon Echo, sasa ni zamu ya kampuni ya Google kuja na  Google home, kifaa hiki kina uwezo wa kujibu maswali mbalimbali kinapolizwa pamoja na kufanya kazi mbalimbali kama vile kuplay muziki, kuwasha tv, kusema saa, kutoa taarifa za hali ya hewa, kusema ratiba ya vipindi vya tv pamoja na ratiba za sinema na mambo mengine mengi.

Advertisement

  • Jina la Toleo Jipya la Android (Awali Android N)

2b

Na jina jipya la android mpya ya sasa nii…? well google imeamua kuomba ushauri wa watu mbalimbali kwenye internet juu ya jina la toleo jipya la Android ambayo awali litwa Android N. Google inategemea kupata jina la android hiyo mpya kwa kutumia maoni ya watu kutoka nchi mbalimbali hivyo kaa tayari labda wewe ndo unaweza ukapata jina jipya la android 7 au Android N.

  • Uzinduzi wa Google Assistant

2a

Google Assistant ni idea mpya ya google ambapo mtu anauwezo wa kuuliza mambo mbalimbali kwa sauti kupitia kifaa chake, Google assistant inauwezo wa kujua mambo mbalimbali kwani unauwezo wa kuifundisha kujibu maswali maalumu unayouliza kama vile “how is my team doing” na Google assistant itagundua ni timu gani unamaanisha, kwa ufupi hii ni kama vile upgrade ya programu ya “Voice now” lakini yenye teknolojia ya hali ya juu zaidi.

  • Programu Mpya ya Allo

3 (1)

Allo ni programu ya meseji ambayo imetengenezwa ndani ya Google Assistant ambayo programu hii inakusaidia pale unapokua unachat na marafiki kwa mfano kama unachat na marafiki kuhusu sinema, programu hiyo ya Allo inawezo wa kujitokeza kati ya chating yenu na kuongezea kuwa inafahamu mahali sinema hizo zinapo onyeshwa kifupi ni kwamba programu hii ya Allo ni kama roboti anaekwepo kutoa msaada pale unapo itajika.

  • Uzinduzi wa Programu Mpya ya Duo

5

Duo ni programu kwaajili ya kupigiana simu za video yani video call lakini programu hii iko tofauti kidogo kwani mtu anauwezo wa kumuonamtu wa upande wa pili hata kabla hajapokea simu hiyo yani hii ni kama vile unamuangalia mtu aliye gonga mlango kabla ya kumfungulia.

[alert type=”info” main_text=”Bado Mkutano unaendela ” second_text=”Pitia Hapa tena ilikuendelea kupata yaliyojiri kwani hayo ni machache tu yaliyojiri hapo jana.” show_close=”false”]

 

 

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use