Twitter Yaondoa Picha Kwenye Hesabu ya Maneno

twitter twitter

Mtandao maarufu wa twitter ambao unao-tumiwa sana na wafanyabiashara wengi duniani hivi karibuni umetoa taarifa ya kuondoa picha katika hesabu yake ya maneno katika post zake, hapo awali picha ilikuwa inaongeza maneno 24 kati ya maneno 140 unayopewa ili kuweka post katika mtandao huo.

Pia mabadiliko mengine ni pale utumiaji anapo jibu tweet na kuanza na @-jina basi jina hilo halito hesabiwa kwenye hesabu hiyo ya maneno 140, twitter imesema inaleta mabadiliko haya ilikuvutia watumiaji wengi pamoja na kuongeza uzoefu wa watumiaji wake katika mtandao huo. Hata hivyo twitter imeonekana kubalika sana hivi karibuni kwani kwenye tarehe zilizopita twitter ilibadilisha mfumo wake wa kuonyesha tweet kwenye mtandao wake huo kutoka (chronological timelines) ambapo mtumiaji ataweza kuona picha zote mpya za watu alio wa follow, kwenda kwenye mfumo wa  (partly-algorithmic system) ambapo mtumiaji ataweza kuona tweet za watu ambao hulike au kuretweet tweet zao mara kwa mara.

Mabadiliko hayo yanategemewa kuja hivi karibuni kwenye platform zote za twitter kuanzia kwenye web na kwenye programu za mtandao huo za android na iOS.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use