in

Instagram Yalipa £7000 Kwa Kijana wa Miaka 10

Instagram

Hivi karibuni kampuni ya instagram ambayo iko chini ya Facebook imelipa Euro 7000 kwa kijana wa miaka kumi ambaye aliweza ku-hack mtandao huo, habari kutoka blog mbalimbali zinasema kijana huyo ambaye alitajwa kwa jina moja la Jani aliweza ku-hack mtandao huo maarufu kwa kufuta comment za watu kwenye mtandao huo.

Hata hivyo ili kuonyesha kwamba anauwezo wa kufanya hivyo Jani alilazimika kufanya zoezi hilo mbele ya wafanyakazi wa instagram na kufuta comment za moja ya akaunti ambayo ilitengenezwa na wafanyakazi hao. Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kulipa ma-hacker ili kuonyesha matatizo mbalimbali ya mtandao huo maarufu, mpaka sasa kampuni hiyo imelipa zaidi ya £3million kwa ma-hacker mbalimbali walio weza kuonyesha matatizo ya mtandao huo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hata hivyo instagram haikuweka wazi jina halisi la kijana huyo, hii ni mara ya kwanza kwa kijana wa miaka kumi ku-hack mtandao huo maarufu wa kubadilishana picha.

Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments