Mwisho wa Wizi wa Simu za Mkononi Tanzania

Mwisho wa Wizi wa Simu za Mkononi Tanzania Mwisho wa Wizi wa Simu za Mkononi Tanzania

Kwa Tanzania pekee wizi wa simu za mkononi umekidhiri sana hasa kwa mikoa mikubwa kama Dar es salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine mikubwa ya hapa Tanzania. Hivi karibuni mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania TCRA imetoa mfumo wa kuzuia matumizi ya simu mbovu, bandia na za uwizi, mfumo huo huitwao kwa kingereza “Central Equipment Identification Register” au CEIR utaanza kutumika hivi karibuni. Watumiaji wa simu za mkononi maarufu kama “Smartphone”na simu zingine zote za mkononi watasajili simu zao ili pale zinapo ibiwa au kupotea ziweze kusitishwa kwa matumizi nchini Tanzania, mamlaka hiyo inasema kua mitandao ya simu itahusika kufanya zoezi hilo la kusajili simu za wateja wake.

Ifuatayo ni barua ya TCRA ilyotolewa kwa umma kutoka kwenye website ya TCRA:

TAARIFA KWA UMMA

Advertisement

MFUMO WA RAJISI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO WA SIMU ZA KIGANJANI (CENTRAL EQUIPMENT IDENTIFICATION REGISTER (CEIR)

UTANGULIZI:

Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani(tablets) – vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.

Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity Register – EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao.

Mfumo huu wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano. Vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano kutumia vifaa vya mkononi.

DOWNLOAD BARUA YOTE HAPA PDF

1 comments
  1. Naombeni msahada kwa hili.nilienda dukani kununua simu lakin ile simu ulikuwa ina matatizo na nilipo Rudi sikupewa msahada wowote na mwenye duka .nifanye Nini hili nipate haki yangu maana Kila kitu kipo mfano listi ninayo.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use